Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozuru ofisi za Mamlaka kwa lengo la kujifunza namna TCRA inavyosimamia mawasiliano. Katika ziara hiyo TCRA na TUZ wameashiria nia ya kuhuisha baadhi ya vipengele vya mashirikiano baina ya taasisi hizo mbili kwa lengo la kuboresha huduma wanazosimamia. Picha zote na: TCRA
Mhandisi Mwandamizi wa Masafa katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Victor Kweka akitoa wasilisho mbele ya Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliozuru ofisi za TCRA Makao Makuu kwa ziara ya mafunzo. TUZ imebainisha kuboresha zaidi utoaji huduma za mawasiliano Zanzibar baada ya ziara hiyo ikiwemo maandalizi ya kupokea mabadiliko ya TEHAMA katika kuboresha sekta ya mawasiliano Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Leseni katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (TUZ) waliofanya ziara ya mafunzo ofisi za TCRA kupata uelewa wa namna Mamlaka hiyo inavyosimamia sekta ya mawasiliano Tanzania.
No comments:
Post a Comment