HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 14, 2022

Dk. Kamani arejesha fomu ya kuwania uspika


Dk. Titus Kamani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Spika.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

ALIYEKUWA Waziri wa Kilimo na Mifungo serikali ya awamu ya nne,
Dk.Titus Kamani amesema ni jukumu la  vikao vya Chama Cha Mapindizi (CCM),katika masuala ya maamuzi ya kumpitisha.

Chama hicho kilifungua pazia la kutoa na urejeshaji fomu za kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamuhuri wa Tanzania baada ya nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Spika wa Bunge hilo na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai aliyejiuzulu hivi karibuni.

Kamani ameyasema hayo jijini Dodoma leo 14,2022 muda mfupi baada ya kurejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo amesema  amerejesha fomu kwa kuwa amekamilisha taratibu na maelekezo yote ya Chama.

" Nimekuja nikiamini kwamba nastahili kuchukua nafasi hii. Katika nafasi zangu zote nilizowahi kuzishika katika uongozi wangu  nategemea sana bila kuwa na watu hakuna linalowezekana pia naamini Mungu kwa kila jambo," amesema Dk. Kamani.

Ameongeza kuwa kimsingi amekamilisha taratibu zote na maelekezo ya Chama hicho.

No comments:

Post a Comment

Pages