HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 08, 2022

Dk. Makundi: Kuna ongezeko la magonjwa yasioambukiza

 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Taifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (COSTECH), Dk.Wilbert Manyilizu akifafanua jambo.


Dk. Emmanuel Makundi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti  wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi , Teknolojia na Ubunifu (COSTECH).

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma


IMEELEZWA kuwa ongezeko la magonjwa yasiyo ambukiza limekuwa na changamoto kubwa nchini hasa katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ambapo tofauti na mtazamo uliopo kuwa wazee ndio wanao ugua magoy hayo.

Pia Wizara  ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto imeombwa kutojikita katika mikakati ya kupambana juu tiba ya magonjwa yasioambukiza na badala yake iendelee kuzingatia kinga zaidi.

Hayo yamesemwa jana na  Dk. Emmanuel Makundi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti  wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), katika warsha iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi , Teknolojia na Ubunifu (COSTECH), amesema kwa mujibu wa Takwimu za kamisheni ya umasikini na magonjwa yasio ambukiza Tanzania zinaonyesha kuna ongezeko kubwa la magonjwa yasiombukiza nchini.

Amesema ongezeko hilo linafikia  hadi asilimia 41ya vifo na majeruhi katika rika mbalimbali.

"Takwimu zinaonyesha  kuna ongezeko kubwa la magonjwa yasiombukiza kwa vijana hususani shinikizo la damu na Kiharusi kwa hali hii ni wazi kuwa sekta ya afya pekee haitoweza kupambana na tatizo hili," amesema Dk.Makundi.

Ameeleza kuwa kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti na zinazohusisha sekta mbalimbali  ili kupambana na tatizo hilo.

Awali akifungua warsha  hiyo mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dk. Wilbert Manyilizu amesema,lengo la warsha hiyo ni kuwashirikisha Wadau wakuu wa matokeo ya tafiti za kisayansi na Teknolojia ili waweze kuwasilisha na kutoa matokeo ya tafiti zao.    

                             
Amesema,COSTECH iliwaita watafiti katika Sekta nne za awali ambazo ni sekta ya Afya,Kilimo,maliasili na mifugo  ili wawasilishe tafiti zao ambazo hufanyiwa kazi na Tume hiyo.

" Tume hii ndio yenye dhamana ya kuishauri Serikali katika masuala ya sayansi na teknolojia ,lengo la kuanzishwa kwa Tume hii ni  kuishauri Serikali katika masuala ya sayanasi na Teknolojia na ubunifu," amesema.

Dk. Manyilizu ameongeza kuwa jukumu kubwa la COSTECH ni kuratibu na kuhamasisha Mambo ya utafiti na ubunifu na majukumu mengine.

Ameyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kusimamia Menejimenti ya maarifa yanayopatikana katika ubunifu na utafiti na baadae kusambaza kwa Wadau na kwamba michakato yote ya kuwatambua na kuwawezesha wabunifu ni jukumu lao.

No comments:

Post a Comment

Pages