HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 05, 2022

Dk. Mukassa: CCM Mkoa wa Dodoma itabaki kuwa Ngome, Rais Samia acha woga fanya kazi


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, Dk. Damas Mukassa akizungumza na waandishi wa habari.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma


MWENYEKI wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, Dk.Damas Mukassa amemwomba Rais Samia  Suluhu Hassan kufanya kazi bila woga na kuachana na baadhi ya  watu ambao wana uchu wa madaraka.

Pia amewataka baadhi ya wanachama na ambao sio wanachama wa chama hicho kuacha,usaliti,uzandiki, majungu,fitna na roho mbaya kwani Rais ni mmoja anatakiwa kuheshimiwa.


Wito huo  ameutoa kufuatia kauli ya jana Rais Samia kudai kwamba kuna baadhi ya wanachama wa chama hicho wamekuwa wakimsaliti katika suala la kukopa kwa ajili ya kuendeleza mitadi mbalimbali ya nchi.

Rais Samia amesema  nchi lazima ikope kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa  ikiwemo ujenzi wa madarasa kwani  fedha za tozo haziwezi kutekeleza mahitaji ya miradi hiyo.

Amesema mkopo ambao Serikali umeupata wa Sh trilioni 1.3 ni mzuri na kwamba haujawahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru.

Akizungumza leo Januari 5, 2022 jijini Dodoma kwa niaba ya chama hicho  Mkoa wa Dodoma leo Januari 5,2022, Mwenyekiti huyo Dk. Mukassa kuhusu kumpongeza Rais kwa  hotuba yake aliyoitoa Januari 4 Jijini Dar es Salaam baada ya kupokea taarifa ya Mpango wa maendeleo wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko19.

Amesema kuwa Ccm Mkoa wa Dodoma itabaki kuwa Ngome  na kwamba wanaunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia.

Dk. Mukasa amelaani makundi yanayowania Urais  mwaka 2025 kwani bado miaka mitatu hawakupaswa kujitangaza na kwamba huo ni usaliti na tamaa na badala yake wamuunge mkono Rais katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo.

" Nampongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya ya kutekeleza miradi mikubwa nimewahi kutembelea madarasa yaliyojengwa na fedha za UVIKO-19, ni mazuri zamani tulikuwa tunayaona katika shule za binafisi tu," amesema Dk. Mukassa.


Aidha Dk Mukassa ametoa wito kwa Wanaccm kuacha majungu,fitina na roho mbaya, kuacha kuharibiana kwani Rais ni mmoja na hivyo aheshimiwe.

No comments:

Post a Comment

Pages