*Mwingine ni Godwin Kunambi
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Tulia Ackson ( kushoto), akikabidhiwa fomu ya kuwania nafasi ya spika (Kulia), ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa (NEC) Shaka Hamdu Shaka.
Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa (NEC) Shaka Hamdu Shaka akizungumza mara baada ya kukabidhi fomu kwa wagombe waliojitokeza kuwania nafasi ya spika.
Na Asha Mwakyonde
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Tulia Ackson,leo Januari 10, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya uspika.
Hivi karibuni aliyekuwa spika wa Bunge hilo na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Job Ndugai alijiuzulu nafasi hiyo na kuachwa wazi.
Pia Dk. Tulia amesema nafasi yake bado ipo pale pale kwani katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawataja watu ambao hawaruhusiwi kugombea kuwa ni Waziri mkuu Mawaziri na Manaibu Makatibu wakuu na wasio wanachama wa chama hicho.
Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kukabidhiwa fomu hiyo
na Katibu msaidizi Mkuu, Idara ya Organaizesheni Solomon Itunda katika Ofisi za Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma, Dk.Akson amesema kuwa ana sifa ya kuwania kiti hicho.
Amesema kuwa amechukua uamuzi huo kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuliongoza Bunge kwani ameliongoza Bunge hilo kwa kipindi cha miaka sita.
" Nitahakikisha nasimamia misingi ya kisheria na kanuni za Bunge ikiwa nitapata nafasi hii," amesema Dk. Tulia
Pia Dk.Tulia amezungumzia utendaji Ndugai amesema kuwa alifanya kazi ya aliongoza Bunge hilo vizuri na kwamba hakuna kilichopwaya kwa kipindi chote alichokuwepo katika nafasi hiyo.
"Shughuli za Bunge Ndugai alifanya vizuri na wala hakupwaya, nami endapo nitapata nafasi hii nitaendelea kusimamia misingi ya haki pamoja na kuliweka Bunge karibu na serikali kwa malengo ya pamoja ya kupata maendeleo kwa wananchi",amesema.
Wakati huo huo Mbunge wa Mlimba Godwini Kunambi naye amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Muda mfupi baada ya kumaliza kuchukua fomu amesema kuwa anataka kutumia nafasi hiyo kuliendesha bunge kwa misingi ya usawa,kanuni na sheria.
Amesema kuwa yeye anauzoefu wa kuongoza na kutokana na taaluma yake ya sheria ataliongoza Bunge kwa viwango vya juu zaidi.
Amesema kuwa amekuwa katibu wa CCM wilaya,amekuwa mwanasheria wa CCM miaka mitano ,amekuwa mkurugenzi wa halimashauri ya Jiji la Dodoma na sasa ni mbunge wa Jimbo la Mlimba.
"Ninaomba ridhaa ya kuwa sipika kwa kuwa uwezo wa kuongoza ninao na nina shahada ya sheria ,shahada ya pili ya utawala hivyo ninaweza kuongoza bunge kwa kufuata misingi ya kikatiba pamoja na kanuni za Bunge.
" Nikipewa ridhaa ya kuwa Spika nitafuata usawa na hakutakuwepo ubaguzi wala upendeleo wa haina yoyote na kila mwenyesifa ya kuwa mbunge atapewa haki yake ya kikatiba,kikanuni na kutaratibu kwa kufuata misingi ya kibunge"amesema.
Amesema walio chukua fomu katika ofisi tatu za chama hicho Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Oganizetion CCM Taifa, Solomon Itunda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa (NEC) Shaka Hamdu Shaka amesema jumlaya waliojitokeza ni 9
katika Ofisisi kuu Dodoma.
Itunda amewaja kuwa Ni Dk.Saimon Ngatunga,Tumsifu Mwansamale,Merkion Ndofu, Dk.Tulia Ackson, Godwin Kunambi na Ambwene Kajula
Amesema katika ofisi ndogo Dar es Salaam waliochukua fomu hiyo Ni watatu ambao ni Patrick Nkandi, Stephen Massele na Hamidu Chamani.
" Kwa upande wake Zanzibar kuanzia saa 8:00 asubuhi hati saa 10 :00 jioni hakuna aliyejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hii," amesema.
Katibu huyo Msaidizi amefafanua mwenye fisa za kuchukua fomu ya kuwania kiti hicho kuwa awe raia wa Tanzania, mwanachama kwa mujibu wa katiba.




No comments:
Post a Comment