Mkuu wa Wilaya ya Muheza Halima Bulembo akifungua moja ya darasa lililojengwa kwa fedha za uviko.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Nassib
Mmbaga akimkabidhi mkuu wa was wilaya ya muheza funguo ya moja ya
madarasa hayo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Muheza, Nassib Mmbaga akielezea namna walivyojenga madarasa hayo.
Na Mwandishi Wetu, Muheza
Halmashauri
ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imekabidhi madarasa 67 yaliyojengwa
kutokana na fedha za Uviko 19 ambayo ujenzi wake umekamilika kwa
asilimia 100 ambapo hadi kukamlikia kwa ujenzi huo wa madarasa hayo
kutasaidia zaidi ya wananfunzi 1440 kupata nafasi ya kusoma vizuri.
Makabidhiano
hayo imefanyika jana katika shule ya sekondari ya Chief Mang'enya na
kushirikisha viongozi wa vyama na serikali pamoja na wakuu wa idara na
wakuu wa shule.
Mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Muheza Nassibu Mmbaga alikabidhi vyumba hivyo 67 pamoja na
madawati kwa mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Muheza Nassibu Mmbaga alisema kuwa halmashauri hiyo
ilipata jumla ya shilingi 1,420,000,000 kupitia mradi namba, 5441_TCRP
kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 67 vya madarasa ya sekondari ambavyo
vimekabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Muheza.
Alisema
kuwa idara ya elimu msingi imepata vyumba vya madarasa 10 vya shule
shikizi tatu na bweni 1 kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum ambapo
ujenzi umekamilika.
Mmbaga
alisema kuwa kwa upande wa sekondari fedha hiyo imesaidia kuondoa
upungufu wa vyumba vya madarasa uliokuwepo wa vyumba 25 na sasa wamepata
ziada ya vyumba vya madarasa 32 ambavyo vitawezesha wanafunzi wote
waliofaulu kuingia kidato cha kwanza 2022.
Alisema
kuwa aidha fedha imesaidia kupata viti na meza ambavyo vitatumiwa na
wanafunzi hivyo hakuna mwanafunzi atakayekaa chini.
Mmbaga
alisema kuwa kwa upande wa shule za msingi imewezesha kujenga bweni 1
la wanafunzi wenye mahitaji maalum ambalo litasaidia watoto wenye
mahitaji maalum kupata huduma ya shule kwa karibu.
Alisema
kuwa fedha hiyo pia imesaidia ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika
shule 3 shikizi ambazo zitaweza kuombewa usajili hali ambayo itasaidia
kuondoa changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kufuata shule.
Awali
akipokea mradi huo Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo amesema
Halmashauri hiyo ilipata kiasi cha fedha shilingi bilioni 1.4ambazo
zilitokana na fedha za Uviko -19 ambapo kiasi hicho cha fedha kimekuwa
faraja kwa wanamuheza kwa kuweza kuwasaidia wananfunzi kuendelea na
elimu wilayani humo.
Bulembo
akipokea madarasa hayo na madawati alisema kuwa fedha hizo zimesaidia
kupata madawati ambayo yatatumiwa na wanafunzi hivyo hakuna mwanafunzi
atakayekaa chini.
Alisema
kuwa wilaya ya Muheza wanaishukuru serikali ya awamu ya sita ya rais
Samia Suluhu kwa kuleta fedha hizo zimesaidia kuboresha miundombinu ya
elimu katika shule za msingi na sekondari.
Bulembo
alitoa onyo kwa wazazi ambao watabainika watoto wao hawajawapeleka
shule katika wilaya hiyo wakibainika watachukuliwa hatua kali ikiwamo
kushtakiwa kwa kuwa serikali imetumia fedha nyingi kujenga madarasa sasa
lazima kila mtoto apate elimu.
alitoa
rai kwa walimu na wanafunzi wa shule hizo kutunza madarasa hayo mapya
ili yadumu kwa muda mrefu kwa kuwa serikali imetoka fedha nyingi katika
ujenzi ambao ni fedha za mkopo.




No comments:
Post a Comment