HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 10, 2022

Filamu ya Binti kuonyeshwa Duniani kupitia NETFLIX


 

Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Filamu ya Binti (2021) yazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania duniani tayri filamu hiyo imeshafanya vizuri kwenye matamasha mbalimbali yakiwemo Pan Afican Film Festival ya Los Angeles, USA, Durban Film Festival ya South Africa pamoja na matamasha nchini Nigeria.

FIlamu  ya Binti imeshinda tuzo ya filamu bora ya mwaka 2021 kwenye tamasha la Filamu la ZIFF-Zanibar na sasa itaonekana kwenye jukwaa la Netflix duniani kote ambapo jukwaa hilo lona watazamaji zaidi ya 200,000,000.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Wanahabari, Mwandishi na Muongozaji wa Filamu hiyo, Seko Shamte amesema Filamu yake tayari imeshaanza kuonekana katika jukwaa la Netflix kuanzia Tarehe 07 Januari, 2022.

“tumepata nafasi ya kuoneshwa Duniani kote, kuna kazi zingine kutoka Afrika hazionekani nje ya Afrika, lakini Filamu yetu imepata bahati ya kuonekana kila pembe ya Dunia bila kikwazo chochote” alisema Bi. Seko Shamte.

Amebainisha, Filamu hiyo imetayarishwa na Wanawake, kuanzia Uandishi wa mswada, Uigizaji, Uongozaji na Uhariri, hivyo mafanikio ya kazi hiyo ni ishara ya ukuaji wa uwezo wa Wanatasnia Wakike nchini.

Ameishukuru Serikali kwa kumuunga mkono katika mafanikio ya filamu yake tangu hatua ya Utayarishaji hadi sasa kuonekana Netflix. Aidha, alimalizia kwa kutanabaisha kuwa, mafanikio ya Filamu hiyo yanaenda sambamba na kuitangaza Nchi Kimataifa.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo amewapongeza Watayarishaji kwa hatua hiyo kwakuwa ni kwa mara ya kwanza Filamu kutoka Tanzania kuoneshwa katika jukwaa hilo, ambapo ni nchi Tatu pekee kutoka Afrika zimeshapeleka Filamu zao, ambazo ni Kenya, Nigeria na Afrika Kusini, ila kwasababu ya ubora, Filamu yetu imefanikiwa kwenda huko.

Dkt. Kilonzo ameeleza kuwa, mafanikio hayo ni mapinduzi kwenye Tasnia ya Filamu nchini, kwani imepiga hatua kubwa katika eneo la Usambazaji, ambapo sasa inasambazwa kupitia jukwaa kubwa linalotazamwa na Watazamaji zaidi ya milioni 200 Duniani.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Eliya Mjatta ametoa rai kwa Wadau wa Filamu na Watanzania kwa ujumla kuiunga mkono filamu hiyo kwa kuitazama katika Jukwaa la Netflix ili kuonesha tija ya kazi hiyo katika Mtandao huo.

Naye Mshindi wa Tuzo ya Muigizaji Bora kupitia Tuzo za Filamu Tanzania 2021, Godliver Gordian amewasahauri Watayarishaji kutayarisha Filamu zenye uhalisia wa Maisha ya Jamii zetu kama ilivyo Filamu ya Binti, na ndio maana imefanikiwa kufika mbali.

Filamu hiyo imefanikiwa kuoneshwa kwenye matamasha makubwa ya Filamu katika nchi za Marekani, Ujerumani, Nigeria, Afrika Kusini na New Zeland.


No comments:

Post a Comment

Pages