HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

January 16, 2022

MAKAMU WA RAIS AKERWA NA UCHAFU JIJI LA DODOMA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akishuhudia takataka zilizoachwa kandokando ya barabara zaidi ya wiki mbili baada ya kukusanywa katika maeneo ya Majengo Jijini Dodoma wakati alipofanya ziara ya kustukiza katika maeneo hayo. Januari 15,2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe wakati alipofanya ziara katika soko la Majengo kukagua zoezi la usafi katika eneo hilo. Januari 15,2022.

 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akitembelea soko la Majengo lililopo Dodoma kukagua utekelezaji wa zoezi la usafi katika soko hilo. Januari 15, 2022.

 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

MAKAMU wa Rais Dkt Philip Mpango ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa jiji la Dodoma kuondoa taka zote zilizozagaa mitaani huku akimwagiza mkurugenzi wa jiji la jiji hilo kuvunja mkataba na kampuni ya usafi wa mazingira ya (GREEN WEST).

Kauli hiyo ya Makamu wa Rais inakuja mara baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kukagua usafi wa mazigira katika maeneo mbalimbali pamoja na soko la Majengo na kubaini mlundikano wa taka nyingi ambazo haziondolewa kwa muda mrefu na kutishia mlipuko wa magonjwa.

Dk. Mpago alisema ni aibu kwa jiji la Dodoma ambalo ndiyo makao makuu ya nchi kuwa na mlundikano wa uchafu katika maeneo ya msoko ambayo yanatumiwa na watu kufanya biashara mbalimbali za vyakula.

“Ni aibu sana na mweshimiwa Rais Samia alitaka kuja hapa nikamzuia nikasema nije kwanza mimi lakini kwa hali niliyoikuta haikubaliki jiji kuwa chafu kiasi hiki naomba taka zote hizi ndani ya muda huo wa wiki mbili ziwe zimeondolewa zote katika maeneo ya mitaa na masoko”amesema Dk. Mpango

Aidha, aliwaagiza wakurugenzi wa majiji yote kuhakikisha kuwa sula la usafi limepewa kipaumbele na kuwa endelevu.

“Jiji la Dodoma ni chafu sana mnashindwa hata na Dar es saalam wao wapo vizuri na kule ndiko kuna fujo sana kwa mfano barabara hii ya kutoka arusha pembezoni ni matakataka tuu ya makaratasi ndani ya hizo wiki mbili nataka msafishe kote na mimi bahati nzuri nakaa hapa Dodoma lazima nitakuja kukagua”alisema

Kuhusu kampuni ya usafi ya Green West alimtka mkurugenzi wa jiji kuvinja nayo mkataba wa kufanya kazi za usafi katika mitaa mbalimbali ya jiji kutokana na kushindwa kutekeleza majikumu yake.

“Nataka mvunje mkataba na kampuni hii haiwezekani wananchi walipa fedha lakini taka haziondolewe katika maeneo yao hadi muda wa wiki mbili nataka pia ipewe adhamu ya kuleta adha kwa wananchi kwa kushindwa kuteleza majukumu yao kwa mujibu wa mkataba”amesema

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru, alisema moja ya chanmoto wanayokabiliana nayo ni uhaba wa magari kwa ajili ya kuzoa taka hizo.

“Mweshimiwa makamu wa rais moja ya changamoto ni uhaba wa vifaa kwani hatuna magari ya kutosha magari yapo manne na moja ndiyo tunalitengeneza lakini mji unakuwa na idadi ya watu inaongeza kila siku lakini tutahakikisha kuwa maagizo yako tuyafanyika kazi ndani ya muda”alisema

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka, alisema atahakikisha kuwa maagizo ya makamu wa Rais yanafanyiwa kazi.

“Tutahakikisha kuwa tunatekeleza chini muda ulitupatia na leo hii viongozi wote wa jiji la wilaya watabaki hapa kufanya vikao ili kupata suluhu ya kuziondoa taka hizi”amesema

No comments:

Post a Comment

Pages