Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Shaka Hamdu Shaka, Katibu msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni, Solomon Itunda akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Chama Cha Mapindizi (CCM), Makao Makuu jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
ZOEZI la uchukuaji fomu za kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .limekamilika leo Januari 15, 2022 ,jumlaya wanachama 71 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Januari 15, 2022, kwa niaba ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Shaka Hamdu Shaka,Katibu msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni, Solomon Itunda amesema kati 71 wanachama wawili hawajarudisha fomu.
Katibu huyo Msaidizi amewataja
waliochukua fomu leo kuwa ni Samweli Magero, Rahimuddin Ismail, Alex Msama, Themistocles Rwegas na Grangany Nyalohaha.
Wengine ni Katibu wa zamani wa Bunge Dk Thomas Kashilila, Waziri wa mifugo wa zamani Luhaga Mpina,Hatibu Madata, Dk Linda Ole Saitabau, Profesa Norman King.
Emmanuel Sendama,Goodluck Milinga, Bibie Msumi, Hilal Seif na Athumani Mfutakamba.
Solomon ameendelea kuwataja wanachama hao waliochukua fomu kuwa ni Mwenda Burton Mwenda, Herry Kessy Josrphat Malima, Adam Mnyavanu, Stella Manyanya na Andrew kevela.
Pia Hussein Mataka, Hatibu Mgeja Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Msalala Mkoani Shinyanga Ezekiel Maige,Wakili Emmanuel Mng'arwe, Aziz Mussa, Wakili Onyango Otieno, Doto Mgasa, Profesa Edison Lubua, Fikiri Said, Profesa Itikija Mwanga na Peter Njemu.
Wengini Ndurumah Mejembe, Godwin Maimu, Johnson Japhet, Mohamed Mmanga, Esther Makazi, Mariam Moja, Joseph Anania, Samweli Xaday, Arnold Peter na Joseph Sabuka.
Pia wengine ni mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa zamani wa Bariafi Andrew Chenge na Dk Titus Kamani, Dk Mussa Ngonyani, Wakili Faraji Rushagama, Hamisi Rajabu,na Asia Abdallah.
Ameongeza kuwa wengine ni Festo Kipate, George Nangale, Barua Mwakilanga, Zahoro Haruna, Andrew Chenge, Thomas Kirumbuyo ,Angelina John na Mhandisi Abdilaziz Jaad Hussein, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, Emmanuel Mwakasaka Mbunge wa Tabora ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na Profesa Hadley Mafwenga ambaye ni Ofisa usimamizi wa fedha kutoka Wizara ya Fedha, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma,Godluck Ole Madeye, Sophia Simba,Juma Hamza Chum na Baraka Byabyato.
Pia Simon Ngatunga, Tumsifu Mwasamale, Merkion Ndofi,Dk Tulia Ackson, Godwin Kunambi na Ambwene Kajula.i Petrick Nkandi, Steven Masele na Hamidu Chamami.
Mchakato huo unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai a Januari 6, mwaka huu.




No comments:
Post a Comment