Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene ameahidi kuboresha maslahi ya mawakili na watendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, baada ya kupokea taarifa ya utendaji ikiwamo kumaliza mashauri 444 na kuokoa Sh. Bilioni 236 za Serikali.
Kadhalika, ameipongeza ofisi hiyo kwa muda wa meizi tisa kumudu kukamilisha mashauri hayo yakiwamo ya madai na usuluhishi.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya siku moja katika ofisi hiyo pamoja na kuzungumza na Menegmenti na watendaji.
"Nimeshangazwa na kufurahishwa sana na taarifa yenu, ndani ya miezi tisa mmefanikiwa kuokoa Sh.bilioni 236 kumaliza mashauri hayo mnastahili pongezi sana" alisema na kuongeza.
"Nitashirikiana na wenzangu kuwasemea mawakili na watendaji mmboreshewe maslahi yenu, mnafanya kazi kubwa na ya kizalendo, tutaendelea kuyafanyia kazi maombi yenu pale mtakapokwama msisite kunifikisha taarifa lakini msideke sana" alisema Waziri Simbachawene.
Akifafanua kuhusu utendaji wa ofisi hiyo, alisema pamoja na yeye mwenyewe kuwa na taaluma ya uwakili lakini wamevunja rekodi waendelee kufanya kazi zaidi na kwamba atawasimamia kuhakikisha utendaji wao.
Akiwasilisha taarifa ya miezi tisa ya utendaji wa awamu ya sita, Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata, alisema ofisi yake ina majukumu makubwa matatu.
Kwanza, Kuishauri Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu mashauri ya madai na usuluhishi yanayofunguliwa dhidi ya serikali nje na ndani ya nchi.
Pili, Kuratibu mashauri ya madai na usuluhishi yanayofunguliwa nje na ndani ya nchi.
Tatu, Kuiwakilisha Serikali katika mashauri hayo ikiwamo kuingilia kati mashauri yanayofunguliwa dhidi ya taasisi binafsi zenye maslahi ya Serikali, mfano; Kampuni ya Simu ya Airtel.
Akifafanua kuhusu Kampuni ya Airtel ofisi yake iliokoa Sh. Bilioni nne zilizodaiwa mahakamani na mlalamikaji.
Mfano wa kesi nyingine ni, iliyofunguliwa na James Mbatia, Job Ndugai dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakipinga utaratibu aliotumia kujiuzuru kwamba haukufuata utaratibu wa kisheria.
Hata hivyo, kesi hiyo wameshinda leo na kumgalagaza Job Ndugai.
January 28, 2022
Home
Unlabelled
Maslahi ya mawakili na watendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuboreshwa
Maslahi ya mawakili na watendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuboreshwa
Share This

About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment