Wazira wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu Prof. Joyce Ndalichako (kushoto), akimkabidhi baadhi ya nyaraka Prof. Adolf Mkenda.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
PROFESA Adolf Mkenda amesema kuwa Wizara ya Elimu na Sayansi na Teknolojia ni nyeti hawezi kubadilisha badilisha mitaala kufanya hivyo ni kulichanganya Taifa.
Pia amesema Wizara hiyo inahitajika kutanya kazi kwa kushirikiana kama timu kwani ndio ndio njia sahihi ya kuboresha elimu nchini.
Hayo ameyasema jijini Dodoma, Januari 13, 2022 wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Mkenda amesema kwa kuzingatia hilo atatenga muda wa wiki tatu kuzungumnza na watumishi wa wizara hiyo.
Ameongeza kuwa watapitia nyaraka mbalimbali muhimu kwa lengo la kufanya uchambuzi yakinifu kwa ajiili ya kuboresha elimu iwe na tija na kwamba ili waweze kufanya kazi vizuri ni lazima washirikiane.
"Niwaombe ushirikiano wenu na msiwe na nidhamu za woga mkiona mambo hayaendi vizuri msisite kusema kwani nyie ni wazoefu katika wizara hii," amesema.
Profesa Mkenda ameongeza kuwa ili kufanikiwa katika kazi yeyote ni lazima kufanya kazi kama timu na kutoa uhuru kwa watumishi wa wizara hiyo kumfuata na kumuelekeza.
Amefafanua kuwa ili kuboresha elimu ya kitanzania haoni tatizola kushirikiana na wataalamu wa elimu katika nchi ni vema wakafanya kazi kama.timu moja.
Kwa upande wake Prof. Ndalichako amewataka watumishi wa Wizara hiyo kumpa ushirikiano waziri wao ili kuendeleza wizara hiyo muhimu.
Amesema kuwa anakabidhi wizara hiyo kwa waziri mgeni huku akiamini kuwa atandeleza mipango mbalimbali iliyopo katika wizara hiyo.
"Aidha amewashukuru wa Wizara hiyo kwa ushirikiano waliompatua kipindi chote akiwa kama waziri wao na kuwaomba watumishi hao waziri mpya kwa ajili ya maendeleo ya nchi.




No comments:
Post a Comment