HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 17, 2022

CCM KILOLO KUJENGA OFISI YA WILAYA YA MFANO NCHI NZIMA

Mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Kilolo Anna Msolla akiwa anafanya usafi katika jengo linalojengwa kuwa ofisi ya CCM wilaya ya kilolo.Viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiwa na wanachama pamoja na wadau wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiangalia mwenendo wa ujenzi wa ofisi ya chama hicho.


 Na Fredy Mgunda, Iringa

 

CHAMA cha mapinduzi wilaya ya kilolo kimesema kinajenga ofisi ya chama ya mfano nchini mzima kwa namna ambavyo wametumia michoro bora na ya viwango vya juu.

Akizungumza na waandishi wa habari,mwenyekiti wa chama hicho Kiliani Myenzi alisema kuwa walianza mchakato huo muda mrefu kwa kuhakikisha kuwa wanajenga jingo la ofisi hiyo kwa viwango vya kimataifa.

Myenzi alisema kuwa lengo la kujenga ofisi hiyo mpya ni kuhakikisha watumishi wa chama wa chama hicho wanafanya kazi katika ofisi yenye ubora na kuongeza ufanisi wa kazi zao kulingana na ofisi wanayofanyia kazi.

Alisema kuwa CCM kilolo imekuwa inawanachama wengi wanaokipenda chama hicho hivyo lazima wajenge ofisi ambayo inaendana na uchumi wa wilaya hiyo ambao wananchi wake wamekuwa wanajituma kufanya kazi.

Myenzi alisema kuwa ofisi hiyo inatarajiwa kukamili hivi karibuni kwa kuwa kasi ya ujenzi inakwenda kwa kasi kubwa na kwa asilimia kubwa kila kitu kimekamili bado umaziaji tu.

Alisema karibu na ofisi hiyo pia utajengwa ukumbi mkubwa wa kisasa kwa ajili ya mikutano na sherehe mbalimbali ambapo pia utakuwa ukumbi wa mfano kwa mkoa wa Iringa.

Myenzi alisema kuwa ukumbi huo utakuwa fahari kwa wananchi na wanachama wa wilaya ya Kilolo na nje ya wilaya ya Kilolo kwa wale ambalo watakuwa wakiutumia kwa shughuli mbalimbali.

Alisema kuwa katika kufanikisha ujenzi huo hawezi kuacha kuwashuku wadau mbalimbali waliochangia ujenzi huo kama vile MNEC Salim Abri Asas,mkuu wa wilaya aliyepita Asia Abdalah,wakurugenzi,wabunge wastaafu na wadau wengine ambao hawajatajwa hapo juu.

Myenzi alimalizia kwa kusema ofisi na ukumbi vikikamilika ndio itakuwa alama yake katika kuwatumikia wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo kwa kipindi akiwa mwenyekiti wa chama hicho.

Alisema kuwa anatarajia kugombea tena nafasi hiyo wakati ukifika kwa kuwa bado anamatarajio mengi ya kuisaidia wilaya ya kilolo kupata maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya hiyo.

Kwa upande wake katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo Remy Sanga alisema kuwa kukamilika kwa ofisi hiyo pamoja na ukumbi kutaongeza kasi ya ufanisi wa kazi kwa watumishi wa chama hicho.

  

Sanga alisema kuwa ukumbi ukikamilika kwa wakati na ubora ambao wanautarajia basi kitakuwa moja ya vitega uchumi vya chama hicho wilaya ya Kilolo.Aaliwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuchangia ujenzi wa ofisi na ukumbi huo ili vikamilike kwa wakati maana ujenzi huo kwa asilimia kubwa unawategemea wadau na wanachama wa chama hicho.

Sanga alimalizia kwa kuwaomba wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wote nchi nzima.

 

 

No comments:

Post a Comment

Pages