HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 11, 2022

TFS:Tupo tayari kutoa watalamu kuelimisha jamii pamoja na miche

 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga akifukia mchanga baada ya kupanda mti katika eneo la Iseni jijini Dodoma.

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAKALA wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS),umesema kuwa upo umejipanga na kwamba upo tayari kutoa miche kwa taasisi,mtu mmoja mmoja pamoja na watalamu wa kwenda kuwapatia elimu.

Haya yamesemwa leo Februari 11,2022, jijini Dodoma na Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Kati wa Uhifadhi wa misitu (TFS), Methew Robert, ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya uzinduzi wa sera ya taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,amesema vitu ninavyofanya uharibifu wa mazingira ni mifugo pamoja na ukame.

Kamishna huyo Msaidizi amesema kuwa baada ya kupanda miti ni vema wakarudi kwenda  kuimwagilia maji na zoezi hili litakuwa endelevu

Amesema si vizuri wakaipanda miti hiyo halafu mwakani wanarudi tena  kupainda sehemu hiyo watakuwa wanapoteza nguvu na fedha ya serikali kwani  kipindi cha mvua Dodoma ni kifupi kuliko cha ukame.

"Kwa niamba ya TFS tumejipanga,  tupo tayari kutoa miche kwa mtu mmoja mmoja, taasisi pamoja na utaalamu wetu ili kuwasaidia,"amesema Robert.

Mbunge wa Pandani Kaskazini Pemba amabye pia ni Balozi  wa Mazingira Mariam Omar Said amesema kuwa amefurahishwa na zoezi la upandaji miti na kwamba ameiwakilisha kamati yake.

Mbunge huyo pia Mwanakamati ya uwekezaji wa Viwanda na Biashara na Mazingira, amesema nasaha zake kwa viongozi wenzake ni kushirikiana na wananchi kuyatunza mazingira.

Naye Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga amesema zoezi la upandaji miti liianza tangu Februari 7, mwaka huu ambapo walipanda miti eneo la Medali na baadae kufanya usafi katika barabara inayoanzia Ilazo Martin Luther kuelekea Wajenzi pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara soko la Mavunde lililopo Chang'ombe Kata ya Chang'ombe.

Amesema matukio hayo wanayafanya sio kwa sababu tlya Dodoma peke yake bali ni kipaumbele na kwamba wanategemea mwamko huo uwepo nchi nzima.

"Kesho sasa ndio kilele cha hii shughuli tunahitimisha kwa kuzindua Sera Mpya ya Mazingira ya mwaka 2021,tunawakaribisha wote muhudhurie, tunanzia barabra ya Chimwaga kuelekea barabara inayoenda Dar es Salaam kupanda miti baada ya hapo tutajiunga na wanaotusubiri viwanja vya Bunge tutaandamana hadi viwanja vya Nyerere square ambapo uzinduzi utafanyika hapo," amesema.

Amesema katika uzinduzi huo wa Sera hiyo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango hivyo wananchi wote wanakaribishwa.
 

No comments:

Post a Comment

Pages