HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 03, 2022

Rais MasterCard Afrika ashuhudia Droo ya 5 NMB MastaBata


Rais Mpya wa Mastercard Kanda ya Africa - Mark Elliott, akibonyeza kitufe cha kompyuta kumtafuta mshindi wa droo ya tano ya 'NMB Mastaba Kivyako Vyako' iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto  ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, Afisa Mkuu wa Biashara na wateja Binafsi, Filbert Mponzi (wa pili kutoka kulia) na  Meneja Mwandamizi wa biashara ya kadi, Manfredy Kayala. 


Rais mpya wa Mastercard Kanda ya Africa Mark Elliott,  Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, (kushoto) Afisa Mkuu wa Biashara na wateja Binafsi, Filbert Mponzi (wa pili kutoka kulia) na  Meneja Mwandamizi wa biashara ya kadi, Manfredy Kayala wakifurahi muda mfupi baada ya kupatikana mmoja wa washindi wa droo ya tano ya MastaBata.

Meneja wa Idara ya Kadi NMB, Sophia Mwamwitwa akibonyeza kitufe kumtafuta mmoja kati ya washindi 100 wa droo ya tano ya MastaBata Kivyako Vyako iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Joram Mtafya.

 

 

NA MWANDISHI WETU

 

RAIS mpya wa MasterCard International Kanda ya Afrika, Mark Elliott, leo Alhamisi Februari 3, ameshuhudia droo ya wiki ya tano ya Kampeni ya NMB MastaBata, ambako washindi 100 wamejishindia jumla ya Sh. Mil, 10, hivyo kufanya pesa zilizotolewa kwa washindi 525 kufikia Sh. Mil. 75 Kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200 zinazoshindaniwa.

 

NMB MastaBata - Kivyako Vyako,' ilianza mwishoni mwa Desemba 2021, ambako kila wiki washindi 100 hutafutwa kupitia droo zinazosimamia na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT). Washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi hujishindia Sh. Mil. 1 kila mmoja, huku wana fainali 30 wakitarajiwa kujinyakulia Sh. Mil. 3 kila mmoja hapo Machi mwishoni.

 

Kampeni hiyo ya wiki 10, inahamasisha matumizi ya kadi za MasterCard, Masterpass QR na Vituo vya Mauzo (PoS), ambako tayari washindi 525 Kati ya 1,080 wamejinyakulia Sh. Mil. 75 kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200 zinazoshindaniwa.

 

MasterCard ni washirika wa kibiashara wa NMB, ambako mwaka jana 2021 Kampuni hiyo iliitunukia NMB Tuzo ya Benki Kinara Katika Kuhamasisha Matumizi ya Kadi, ambako Rais Mark Elliott, ameshuhudia moja ya droo za kampeni mbalimbali za kuhamasisha matumizi hayo yasiyohusisha pesa taslimu.

 

Rais Elliot ambaye ni mpya madarakani, ametembelea NMB kujionea huduma mbalimbali na shughuli za kiutendaji na kiuendeshaji kwa jumla, ambako amekiri kuvutiwa na Kampeni ya MastaBata na huduma za benki hiyo kwa ujumla.

 

Akizungumza kabla ya droo, Meneja wa Idara ya Kadi NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema tayari washindi 400 wa droo za kila wiki walishatwaa Sh. Mil. 40, huku washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi Januari wakijinyakulia Sh. Mil. 25, hivyo kupatikana kwa washindi 100 wa droo ya 5, kuigawa kampeni hiyo nusu kwa nusu kuelekea 'Grande Finale' mwishoni mwa Machi mwaka huu.

 

"Tayari washindi 400 wamenufaika na Sh. 100,000 kila mmoja kwa droo za mwisho wa wiki, sambamba na washindi 25 wa Januari waliojinyakulia Sh. Mil. 1 kila mmoja. Tuko katikati ya kampeni yetu, kwani tumebakisha wiki 5, droo moja ya mwisho wa mwezi Februari, pamoja na fainali mwishoni mwa kampeni hii.

 

"Wito kwa Watanzania ni kuchangamkia fursa za kujishindia motisha hizi. Wenye akaunti waendelee kutumia kadi zao kufanya miamala, malipo na manunuzi, na wale wasio na akaunti, wajitokeze matawini kufungua na kuomba kadi, ili kukidhi kigezo kikuu cha ushiriki wa kampeni hizi na kunufaika na zawadi za pesa taslimu," alisisitiza Mwamwitwa.

 

Droo hiyo ilifanyika chini ya usimamizi wa Mkaguzi wa GBT, Joram Mtafya, ambaye aliwahakikishia wateja wa NMB kuwa, kampeni hiyo inaendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zinazotambuliwa na bodi yake na kwamba uwepo wake hapo ni mfululizo wa utekelezaji wa majukumu yao ya kuhakikisha washindi wanapatikana kihalali, huku akiwatoa  hofu wateja wote.

No comments:

Post a Comment

Pages