HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2022

Rais Samia: Nasikia sauti ya Hayati Dk.Magufuli inanitaka niendeleze miradi

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa atahakikisha anaiendeleza miradi yote iliyoachwa na mtangulizi wake Hayati Dk. Joseph Magufuli huku akiwataka Watanzania kuitunza miradi hiyo.

Hayo ameyasema  leo jijino Dodoma, Febuari 9, 2012,  katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa  Kilomita 112.3 amesema anaisikia sauti ya Dk. Magufuli ikimtaka kuendeleza miradi aliyoiacha.

Pia amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara ambapo gharama ya ujenzi wa kilomita 1 ni shilingi bilioni 1.2 hadi 1.5 hivyo amewaomba watanzania kuzitunza.

Aidha ameongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo unaenda kufungua masoko hivyo ametaka ujenzi huo ukamilike kwa wakati kwani utatoa fursa mbalimbali hivyo watanzania kujiongezea kipato.

"Ndugu zangu Benk kudhamini miradi 11 hii inadhihirisha kweli hii ni Benk kwa ajili ya waafrika,"amesema

Amesema kilomita moja ni shilingi  bilioni 1.2 hadi 5 hivyo amesema Serikali inatumia fedha nyingi hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania  Kutunza Miundombinu na kuacha mambo ya hovyo yanayofanywa Katika uharibifu huo.

Kadhalika Rais Samia amesema Serikali inajenga  barabara 23 kwa fedha za ndani huku 13 kazi ikiwa inaendelea.

"Tunashukuru sana Serikali ya awamu ya tano kuleta vuguvugu hili pamoja na kuungwa mkono na Benk ya Maendeleo na hawapo katika barabara wapo pia katika maji na umeme tumewaomba kutusaidia katika uwekezaji wa watu,"amesema

Rais Samia ameeleza kuwa Hayati Rais Dk.Magufuli amemuachia urithi mzito ambapo  ameahidi kuyafanyia kazi  mawazo yote aliyoyaanzisha kuyatekeleza kwa ukamilifu.

Ameongeza  kwamba moja kati ya mawazo hayo hivyo anahitaji  kuungwa mkono na African Bank kwa lengo la kwenda  kukamilisha mradi huo kama alivyotaka Hayati Rais Magufuli.

"Tangu asubuhi siku ya leo nasikia sauti ya mtangulizi wangu ikinielez  kuhusu miradi aiyoiacha ikiwemo ya kuhamia Dodoma na mingine ikiwemo huu wa barabara ya mzunguko wa nje Dodoma," amesema Rais Samia.

Rais Samia ameeleza kuwa wameweka  jiwe la msingi la mradi huo  lakini kàzi hiyo waswahili wanasema ukiona vinaelea vimeundwa na kwa bahati nzuri muundaji wa suala hilo aliyetekeleza maono ya Taifa kuhamia Dodoma aliyetakuipanga Dodoma ,kwa bahati mbaya Mungu amemchukua.

Pia amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara ambapo gharama ya ujenzi wa kilomita 1 ni shilingi bilioni 1.2 hadi 1.5 hivyo amewaomba watanzania kuzitunza.

Aidha ameongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo unaenda kufungua masoko hivyo ametaka ujenzi huo ukamilike kwa wakati kwani utatoa fursa mbalimbali hivyo watanzania kujiongezea kipato.

"Ndugu zangu Benk kudhamini miradi 11 hii inadhihirisha kweli hii ni Benk kwa ajili ya waafrika,"amesema

Amesema kilomita moja ni shilingi  bilioni 1.2 hadi 5 hivyo amesema Serikali inatumia fedha nyingi hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania  Kutunza Miundombinu na kuacha mambo ya hovyo yanayofanywa Katika uharibifu huo.

Kadhalika Rais Samia amesema Serikali inajenga  barabara 23 kwa fedha za ndani huku 13 kazi ikiwa inaendelea.

"Serikali ya awamu ya tano imeleta  vuguvugu hili ambalo  limeugwa  mkono na Benki ya Maendeleo ambao wameisaidia barabara na katika sekta ya  maji na umeme tuna washukuru kuwaomba kutusaidia katika uwekezaji wa watu,"amesema

Awali akiwasilisha taarifa ya Mradi huo,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi  Rogatus Mativila amesema lengo la kujenga barabara hiyo ni kupunguza msongamano katika Jiji la Dodoma.

Amesema jumla ya gharama ya Mradi huo ni shilingi bilioni 249 ambazo ni Kwa ajili ya fidia na ujenzi ambapo amedai  kuna miradi midogo midogo kama ujenzi wa vituo vya afya,ununuzi wa ambulance wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Mtendaji huyo wa TANROADS ameeleza kuwa lengo ni kupunguza msongomana mkubwa wa magari katika Mkoa wa Dodoma ambao ungesababishwa na muingiliano wa magari yanayosafiri kupitia mjini.

Ameeleza kuwa barabara hiyo ina umbali wa Kil 20 kutoka katikati ya Jiji la dodoma ikiwa imegawanywa kwa wakandarasi wawili ambao ni M/sAVIC INTL Project  na China Civil Engineering Construction Cooperation zote kutoka Jamhuri ya watu wa China.

 Alifafanua kuwa awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa Kilomita 52.3 kupitia Nala,Veyula,Mtumba na Ihumwa wakati awamu ya pili itahusisha Kilomita 60 kupitia Ihumwa, Matumbulu na Nala.

Kwa upande wake,Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AFDB) Dk.Akinwumi Adesina amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo amedai wanaamini Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji.

Amesema Benki hiyo  imewekeza kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali yenye  thamani ya  Dola za kimarekani bilioni 2.5.

"Miaka kadhaa iliyopita nilikaa na kuzungumza na rafiki yangu,mtu wa watu hayati Dk.Magufuli kuhusu kutekeleza mradi huu ,Kwa bahati mbaya hayupo tena lakini Kutokana na ushirikiano wake kwetu tunaahidi kuendelea kishirikina na watanzania kwa miradi mingi zaidi,"amesema.

Naye,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iliona kuna umuhimu wa Kujenga barabara hiyo kutokana na ongezeko la watu pamoja na Dodoma kuwa Makao Makuu hivyo magari yanayoingia na kutoka kuwa mengi.

"Tunatoa shukrani kwa Benki ya Maendeleo ya  Afrika kwa kutekeleza mradi huu,imetoa fedha nyingi katika miradi ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ya wakandarasi,

Bila kuwa na Mahusiano mazuri hili lisingetokea niipongeze Wizara kwa mradi huu mkubwa ni ubunifu mkubwa  na utafungua fursa nyingi hivyo ,"amefafanua.

No comments:

Post a Comment

Pages