Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi nchini leo tarehe 08 Februari, 2022. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Wakuu wa Mikoa, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa katika Kikao Kazi cha Wakuu hao wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 08 Februari, 2022.
No comments:
Post a Comment