HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 09, 2022

TFS yatakiwa kuwasiliana na jiji kupata hati za Hekta 56,000



 

 

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro akifukia mchanga mara baada ya kuupanda.

 

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk.Andrew Komba (kulia), wa kwanza kwa wanaopanda mti akipanda mti huo.



Na Asha Mwakyonde, Dodoma

 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Damas Ndumbaro ameelekeza  Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS), kuwasiliana na Halmashauri ya jiji la Dodoma ili hekta 56,000 zipatiwe hati mipaka yake ijulikane isije ikavamiwa baada ya miaka 20 mbele.

Pia amesema gharama ya kutengeneza Oksijeni maabara kwa mtu mmoja kwa kipindi cha mwaka mmoja ni milioni 270  hivyo hukuna mtanzania atakayeweza kuinunua.

Waziri huyo ametoa maelekezo hayo leo jijini hapa wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye zoezi la upandaji miti linaloendelea katika wiki ya uzinduzi wa sera ya taifa ya Mazingira inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 12 jijini Dodoma, amesema wakishapata hati hakuna atakaye vamia.

Amesema  TFS ni Taasisi ya Serikali kila mtu ataheshimu hivyo taasisi hiyo  waendelee kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

"Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira muendelee kushirikiana Wizara ya Maliasili na Utalii kwani siai tuna mazingira huwezi kutenganisha misitu na mazingira, kazi ya misitu ni kuweka mazingira Safi," amesem Dk. Ndumbaro.

Pia waziri huyo amefafanua kuwa  watu wengi hawajui kazi ya misitu ndio makao makuu ya nyuki ambapl anatengenezea mazao saba na kwamba bila nyuki hakuna kilimo.

Amesema nyuki wote wakiuawa baada ya miaka mitano  hakutakuwa na chakula hivyo nyuki hao wanatoka kwenye miti ndio maana wanaipanda miti hiyo.

Waziri Ndumbaro ameeleza kuwa mfugaji anategemea misitu na kama hakuna mvua hakuna misitu kutakuwa na ukame na mifugo hiyo itakufa.

Misitu inafanya kazi mbili inachukua hewa ya Ukaa inabadilisha kuwa oksijeni ambayo binadamu huitumia bila oksijeni hiyo watakufa.

Naye Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo amesema Mazingira ni dhana pana  na ina masuala mabalimbali yaliomo ndani yake ila sehemu kubwa ya mazingira ni Misitu.

Amesema tuanapoongelea misitu tunagusa sekta ndogo ya nyuki ili kufikia malengo hayo na ndio maana tuko hapa  tukifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupanda miti

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk.Andrew Komba kuwa wamewwka alama Iyumbu kwa kupanda miti na kwamba katika wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira walipanda miti hiyo.

Ameongeza kuwa katika tukio hilo walilolifanya la kupanda miti  lilianza tangu Februari 7 na  linatarajiwa kuhitimishwa Februari 12,mwaka huu ambapo wamefanya shughuli mbalimbali za  kupanda miti katika eneo la Medali na  kufanya usafi katika maeneo ya barabara ya Ilazo inatokea Wajenzi.

"Sehemu hii ya Iyumbu wenzetu wa Halmashauri ya jiji la Dodoma wametenga eneo hili kama eneo la hifadhi linapaswa kupandwa miti wenyewe wanasema ni eneo la kijani (Green Park),eneo la kijani,"amesema.

Mkurungenzi huyo amesema kesho watakuwa soko la Chang'ombe kutoa elimu kwa jamii namna bora ya kusimamia taka na kuzitenganiasha kwa kwa sasa taka hizo ni mali.

Ameeleza kuwa wataoa elimu ya kutenganisha taka ngumu na zile za vyakula na kwamba taka hizo zinaweza kutenganezwa kuwa mkaa kwa baadhi yao.

Dk. Komba amesema katika zoezi hilo la upandaji miti na kutanya usafi wameshirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo wananchi na wanahabari.

No comments:

Post a Comment

Pages