HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 08, 2022

Serikali ya mkoa wa Dodoma kuwalipia ada wanafunzi waliofanya vizuri 2021



 Mkuu wa Dodoma Anthony Mtaka  akizungukatika hafla ya utoaji tuzo  kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri  matokeo ya kidato cha nne 2021.


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema kuwa serikali ya Mkoa huo itawasomesha wanafunzi 43 wa kidato cha tano na sita kwa waliofanya vizuri kidato cha nne 2021 kwa shule za serikali.

Pia Mtaka amenunua alama "A" kwa shilingi 5000 lengo likiwa ni kuwapa motisha walimu wa masomo ambayo wamepata alama hiyo na kila mwanafunzi aliyepata alama ya "A" ya pointi 7 hadi 9 kwa wanawake na kwa wanaume pointi 9, serikali ya Mkoa itawalipia ada.

Haya aliyasema jana katika hafla ya utoaji tuzo  kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri  matokeo ya kidato cha nne 2021,Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa watagharamia, vifaa vya shule pamoja na kulipa kwa kipindi cha miaka miwili.

Alifafanua kuwa wanafunzi hao 43 kati yo wasichana 35 na wavulana ni 8 kutoka shule za sekondari za Mpwapwa,Lukundo,Mlowa barabarani, Dodoma, Msalato girls, Mtera Dam, Gode dode.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema wanataka wawe na ushindani kwenye uchumi hivyo lazima wawekeze katika suala la  elimu kwani hakuna nchini duniani iliyoendelea bila kuwekeza katika elimu.

" Kazi ya serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi hawa ni kuwezesha na kuhakikisha ada na vifaa vinapatokana, wajibu wa mzazi utabaki katika suala la sare za shule, mzazi mtoto wako akipangiwa shule njoo na barua yake tuletee sisi tunampatia vifaa na pamoja na kulipa ada.Na leo tunawapatia madaftari 9 kila mmoja, " aliongeza Mtaka.

Kamati ya kitaalamu tuone namna ya kufanya mitihani ya mara kwa mara ya vitendo na kama mzazi anauwezo wa kumuwezesha mtoto wake  atafute mwalimu amuwezeshe kwani sifuri atakayoipata haita nizuia, haitamzuia afisa elimu kula itakaki kwenye familia yako,' alisema.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwata maofisa elimu kuwapa heshima, kuwatunza walimu na kuwafisia pale wanapostahili sifa.

"Na nyie wanafunzi mnao wajibu wa kusoma kila matokeo ni ya wanafunzi na wazazi wao hivyo mjitahidi kusoma," alisema Mtaka.

Awali Katibu Tawala wa mkoa huo Fatma Mganga alisema kuwa wageni waliohudhuria hafla hiyo ni 900 na kwamba inaashiria kuwa wameanza safari ya sekta ya elimu kwenda kufanya makubwa.
 

No comments:

Post a Comment

Pages