Mkuu wa Idara ya mazingira kutoka jiji la Dodoma Dickson kimaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufanya usafi Kata ya Nzuguni jijini Dodoma.
Na Asha Mwakyonde, Dodoma
WANANCHI wenye maeneo ambayo hawajayaendelezwa wametakiwa kuyaendeleza na kuyafanyia usafi na kama wakishindwa wawaachie watu wenye uwezo la sivyo utaratibu wa kisheria utafuata wa kunyang’anywa maeneo hayo.
Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Mkuu wa Idara ya mazingira kutoka jiji la Dodoma Dickson kimaro, wakati wa kufanya usafi katika Kata ya Nuguzni ikiwa ni kuelekea katika maadhimisho wiki ya mazingira amesema kuwa Mkurugenzi wa jiji tayari alishatoa maelekezo ya maeneo hayo mmiliki akishindwa utaratibu wa sheria utafuata.
“Nawashukuru sana wananchi wa Kata ya Nzunguni kwa kufanya usafi katika barabara hii ya kutoka Martin Luther na kuelekea kule Ilazo na kufika Wajenzi na usafi huu tutaendelea nao.Pia nawashukuru wanafunzi wote waliojitokeza kufyeka nyasi na kufanya usafi,”amesema Kimaro.
Amesema wapo katika wiki ya maadhimisho ya uzinduzi wa sera ya Taifa mazingira ya mwaka 2021 ambapo anatrajiwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Mpango na kwamba katika wiki hiyo kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za mazingira zikiwamo za kupanda miti.
Mkuu huyo wa Idara ya Mazingira ameongeza kuwa suala la usafi ni la tabia ambalo linatakiwa kuanza na wananchi wenyewe kipande kilichofanyiwa usafi kinaonekana kuwa na muonekano mzuri Dodoma ni Makao makuu ya nchi sula hilo la usafi ni chachu kila mmoja ahakikishe mita tano kutoka nyumba yake hadi kwa jirani yake kumefanyiwa usafi.
Kimaro amefafanua kuwa kuna baadhi ya watu wamepewa viwanja kwa muda mrefu na wameshindwa kuviendeleza na maelekezo waliyopewa katika hati zao za viwanja hivyo yanaelekeza baada ya miaka mitatu wawe wameayaendeleza.
Amesema kuwa kwa wafanyabiashara za mighawa, hoteli,nyumba za kulala wageni wametakiwa kufanya usafi kwa sababu usafi ni ustaarabu na una anza na mtu mwenyewe.
Zaidi ya asilimia 75 hadi 80 ya magonjwa yanayowakupata wananchi yanatokana na uchafu hiyo usafi unapofanyika ni njia mojawapo ya kujinginga na magonjwa mablimbli.
Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Nzuguni C Idris Bale, ameushukuru uongozi wa jiji hasa Idara ya Mazingira kwa ushirikiano wano na kwamba kwa upande wake ameahidi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao yaliyowazunguka kwa kushirikiana na WananchiSerikali wake.
“Tunaahidi kwa hali hii umlioiacha ya mazingira safi na sisi tutaendelea na utaratibu huu na hata mkija kurudi tena hamtakuta hali ya awali, pia nashukuru waandishi wa habari kwa kuwa tumekuwa wote tangu saa kumi na mbili asubuhi na kuweza kuhabarisha umma katika masuala ya usafi,”anasema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa shina Ilazo Mbuyuni Erick Mahundi amesema kuwa amefurahishwa na usafi huo uliofanyika katika kata hiyo na kwamba kwa nafasi yake atahakikisha atawahamasisha wananchi wake kufanya usafi.
No comments:
Post a Comment