HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 16, 2022

Serikali yatenga bil.1 kwa ajili ya wabunifi wa MAKISATU


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda,amesema kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 1 kwa ajili kuwaendeleza wabunifu watakaotambuliwa kupitia wiki maonesho ya Kitaifa ya Sanyans, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), ambayo yatafanyika mwaka huu mkoani Dodoma.

Wiki hiyo ya maonesho itaafhimishwa jijini hapa kuanzia Februari 15 hadi 20 Mei mwaka huu ambayo itaenda sambamba na kilele cha NAKISATU.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo Februari 16,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya  Wiki  ya Ubunifu na Mashindano ya MAKISATU kwa mwaka 2022

Amesema  lengo la serikali imetenga kiasi hicho cha fedha ni kuendeleza bunifu zitakazoibuliwa kupitia mashindano ambayo yatahusisha mikao 17.

Waziri huyo ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya,Arusha,Iringa,Mwanza,Tanga,Kilimanjaro,Morogoro, Njombe, Kagera, Mtwara na Kigoma,Mara, Ruvuma na mingine kutoka Zanzibar.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa  mikakati ya serikali ya awamu ya sita ni kuongeza hamasa ya matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo za kutatua changamoto za kiuchumi na kwa Watanzania wabunifu.

"Wiki  hii ya ubunifu imeandaliwa kwa kushirikiana na program ya Funguo ya shirika la UNDP ambao nia yake ni kuwatambua wabunifu wa masula ya sanyansi na teknolojia," amesema Prof.Mkenda.

Ameongeza  washiriki wa mashindano hayo watatoka katika makundi Saba huku akiyataja kuwa ni shule za msingi, sekondari, vyuo vya Ufundi Stadi, vyuo vya Ufundi, vyuo vikuu, Taasisi bza Utafiti na Maendeleo na mfumo usio rasmi.

Aidha amefafanua kuwa waneongeza muda wa usajili wa ubunifu wa Mashindano hayo hadi Februari 28, ambapo awali ilikuwa mwisho Februari 10, mwaka huu kutokana na watu wengi kuhitaji kushiriki.

" Hadi kufikia jana Februari 15, tayari tumeshasajili wabunifu zaidi ya 480 kwa ajili ya Mashindano nichukue fursa hii kuwatangazia wabunifu kuwa tumeongeza muda wa usajili hadi For 28, mwaka huu," ameeleza Prof. Mkenda.

“Usajili wa washiriki wa MAKISATU 2022 ulianza rasmi tangu tarehe 27 Desemba, 2021 na usajili huo unaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikishirikiana

Amesema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inayosajili wabunifu wa makundi ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Utafiti na Maendeleo.

Pia ameongeza kuwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inayosajili wabunifu wa makundi ya Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi na wale wa Mfumo usio rasmi Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi linalosajili wabunifu wa kundi la Vyuo vya Ufundi.

Aidha amesema ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara inasajili wabunifu wa makundi ya Shule za Msingi na Shule za Sekondari.

Prof. Mkenda amesem katika kilele hicho kutakuwa na maonesho ya teknolojia na bunifu mbalimbali, bidhaa na huduma zinazotolewa na taasisi zitakazoshiriki zikiwemo taasisi za kitafiti na maendeleo, Vyuo Vikuu, kumbi za ubunifu, taasisi za kibiashara, wakala za Serikali, Wizara na Taasisi binafsi na pia katika kilele hicho kutakuwa na utoaji tuzo kwa wabunifu 21 walioshinda MAKISATU.

Amesema wiki ya MAKISATU imelenga kuibua, kutambua na kuendeleza jitihada zinazofanywa na wabunifu wa Kitanzania na kuhamasisha matumizi ya Sayansi Teknolojia na ubunifu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Waziri huyo ameeleza kwamba kupitia  MAKISATU 2019, 2020 na 2021, Wizara imefanikiwa kuibua na kutambua wabunifu wachanga 1,785.

Amesema kupitia wabunifu hao bunifu 466 zilikidhi vigezo, zimetambuliwa na kuhakikiwa na kati ya hizo bunifu mahiri 200 tayari zinaendelezwa na Serikali ili kufikia hatua ya kubiasharishwa.

“kati ya bunifu zinazoendelezwa na Serikali, 26 zimeshafikia hatua ya kubiasharishwa, wakati 95 ziko katika hatua ya Sampuli kifani (prototype) na nyingine katika hatua za awali za kuandaa sampuli kifani” amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga amesema kuwa katika wabunifu walioibuliwa wanalelewa katika vyuo vikuu na vyuo mbalimbali hapa nchini na kuendeleza na kulea bunifu hizo ili zifikie hatua ya kuingizwa sokoni.

No comments:

Post a Comment

Pages