Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bw. Edward
Nyamanga akifungua Warsha ya Uhamasishaji wa Utekelezaji wa Mpango –
kazi kitaifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwenye Uchimbaji mdogo wa
Dhahabu (2020-25) iliyofanyika jijini Dodoma leo Machi 15, 2022.
Washirki wa Warsha ya Uhamasishaji wa Utekelezaji wa Mpango – kazi kitaifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwenye Uchimbaji mdogo wa Dhahabu (2020-25) wakiwa katika picha ya pamoja na
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bw. Edward Nyamanga wakati akifungua warsha hiyo jijini Dodoma leo Machi 15, 2022.
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
Sekta
ya wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini hutumia tani 18.5 za Zebaki
kila mwaka bila kuzingatia tahad hari kinasi kinachoweza kuathiri afya
za wananchi na mazingira hali inayoweza kuathiri ustawi wa maendeleo
endelevu ya nchi yetu.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira),
Edward Nyamanga wakati akifungua Warsha ya Uhamasishaji wa Utekelezaji
wa Mpango – Kazi Kitaifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwenye
Uchimbaji mdogo wa Dhahabu (2020-25) jijini Dodoma leo Machi 15, 2022.
Alisema
kuwa Licha ya faida kubwa inayopatikana kutokana na sekta hii, shughuli
za wachimbaji wadogo zimeibua changamoto nyingi kwa afya ya binadamu na
mazingira zikiwemo umwagaji maji yenye sumu kwenye mazingira.
Pia
alisema kuwa mazingira yanakabiliwa na uchafuzi wa hewa unaotokana na
uchomaji holela wa dhahabu, ukataji wa miti mikubwa kupata magogo ya
kujengea mashimo na wakati huo binadamu kufanya uchenjuaji wa dhahabu
bila kutumia vifaa kinga unaweza kusababisha madhara ya kiafya.
“Shirika
la Afya duniani (WHO), limeitaja Zebaki kuwa ni miongoni mwa vyanzo 10
hatarishi kwa afya ya binadamu na kutokana na hali hiyo, Jumuiya ya
kimataifa ilipitisha Mkataba wa Minamata mwaka 2013, wenye madhumuni ya
kulinda afya ya binadamu dhidi ya madhara ya uchafuzi wa mazingira
unaotokana na kemikali hiyo.
“Madhara
makubwa ya kiafya yatokanayo na Zebaki ni pamoja na kuathirika kwa
mfumo wa neva, miguu na mikono kufa ganzi, kukosa nguvu, misuli kulegea,
figo kuathirika, uono hafifu, kupoteza uwezo wa kusikia na kuongea,
mimba kuharibika, kuzaa watoto wenye ulemavu wa akili, kupoteza
kumbukumbu, kukosa usingizi kwa muda mrefu na kiharusi,”
alitahadharisha.
Kwa upande
mwingine Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kuwa katika kuhakikisha
tunalinda afya ya binadamu dhidi ya madhara yatokanayo na Zebaki,
Tanzania ilishiriki kikamilifu katika majadiliano ya kuanzishwa kwa
Mkataba wa Minamata, kutia saini makubaliano ya Mkataba huo mwaka 2013
na kuuridhia mwaka 2020.
Kwa
mujibu wa Ibara ya saba (7) ya Mkataba wa Minamata inazielekeza nchi
wananchama kupunguza au kusitisha kabisa matumizi ya Zebaki, hivyo
Tanzania ilitekeleza mradi wa miaka miwili wa kuandaa Mpango Kazi wa
Taifa wa miaka Mitano (5) (2020-25) wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki.
Alisema
mradi huu ni nyenzo mojawapo ya kupunguza na iwapo itawezekana
kuondosha kabisa matumizi ya zebaki katika shughuli za uchimbaji mdogo
wa dhahabu kwa kuhamasisha matumizi ya teknolojia mbadala ili kulinda
afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla. Alilishukuru Shirika la
Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kwa msaada wa rasilimali fedha na
Utaalamu katika kufadhili mradi huo.
Warsha
hiyo imeshirikisha washiriki kutoka wizara za kisekta na taasisi za
Serikali zinazohusiana na shughuli za uchimbaji mdogo wa dhahabu
unaotumia kemikali ya Zebaki.
No comments:
Post a Comment