Taarifa hiyo imethibitishwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Lughano Kusiluka, ambaye ametangaza kifo cha Prof. Ngowi na Dereva wake, waliofariki kwa ajali ya gari wakiwa njiani kwenda Kampasi Kuu Morogoro.
"Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine.
"Taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu. Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito.
Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imetoka eneo la Mlandizi mkoani humo ikihusisha magari matatu.
"Ni kweli ajali imetokea leo saa 12 asubuhi ikihusisha magari matatu aina ya Noah, Land Cruiser alilokuwa anasafiria yeye na lori ambalo ndio chanzo cha ajali lilihama njia na kuiangukia Noah ubavuni kisha kuilalia gari ya Ngowi," amesema Lutumo.
Lutumo amesema hadi wanamtoa eneo la tukio alikuwa bado mzima akiwaishwa Hospitali ya Rufaa ya Tumbi Mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment