HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 10, 2022

Profesa Mbarawa aipa neno TPA kupiga hatua



Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa kujilinganisha kimataifa ili izidi kupiga hatua kubwa zaidi.


Hayo ameyasema Jijini humo wakati akipokea meli kubwa iliyotoka Japan yenye magari  ya 4,041 ambapo kwa bandari ya Dar es Salaam ni mara ya kwanza kupokea meli yenye magari mengi kiasi hicho.

Amebainisha kuwa amesema kuwa kwa sasa magari yatakaguliwa huko yanakotoka ili kupunguza mlundikano wa mizigo isiyo ya lazima pamoja na makontena yaliyokaa bandarini mda mrefu yapelekwe bandari na kama meli ilikuwa inashusha mzigo kwa siku mbili itumie siku moja

 Amekitaka kitengo cha masoko cha TPA kutoka nje kuitangaza bandari pamoja na kuhakikisha kuwa bidhaa za wadau wao zipo salama ili bandari iendelee kupata sifa nzuri na kuingiza mizigo mikubwa zaidi.

 Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza bandari ya Dar es Salaam kila anapokuwa kwenye mikutano ya kimataifa na wao kama wasaidizi wake watahakikisha kuwa wanafanya kazi kwa bidii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Erick Khamis amesema magari zaidi ya 4000 yaliyoletwa na Meli kutoka Japan asilimia 27 yanabaki hapa nchini na asilimia 70 yanaenda nje ya nje ikiwemo Sudan kusinu, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi.

Aidha amesema Meli zinazoweza kutia nanga bandari ya Dar es Salaam zinaweza kubebe gari hadi 8000 hivyo kadri siku zinavyokwenda Meli zenye mzigo mkubwa zitazidi kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam kutokana na Tanzania kuaminiwa na nchi nyingine kubebe bidhaa zao.

“Tarehe 6 na 7 mwezi huu tumepokea meli nne za magari ukijumlisha na meli iliyoingia leo tutakuwa tumepokea gari zaidi 8000 kwa siku tatu hivyo kasi ya maendeleo ni kubwa na sisi kama TPA tunaendelea kujipanga “Amesema Mkurugenzi Eric

No comments:

Post a Comment

Pages