HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 06, 2022

RC Makalla alielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalum kuwakamata Panya Road



 
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
 
Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam Mkuu wa Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  kuanza mara moja msako wa kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya wizi na unyang’anyi wa kutumia silaha maarufu  'Panya road 'na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Maagizo hayo ameyatoa  baada ya kutokea matukio ya uhalifu yaliyofanywa na Panya road  katika maeneo mbalimbali ikiwemo Tabata, Chanika, Zingiziwq na Kunduchi yakihusisha vijana wa miaka kati ya 13 hadi 21.

 RC Makalla  ametoa maelekezo hayo jijini humo katika kikao kazi cha kukabiliana na uhalifu huo kikihusisha na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Wilaya, Wakuu wa Usalama, Makamanda wa Wilaya zote za Kipolisi, Wakuu wa Vituo vya Polisi na Maafisa Polisi Jamii wa Kata na kuwapatia maelekezo.

RC Makalla ameelekeza Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi za Wilaya kufanya kikao na Wenyeviti wote wa Mitaa husika kujadili ajenda ya kudhibiti uhalifu huo.

 Ameelekeza OCD, Wakuu wa Vituo vya Polisi na Polisi Jamii kuongeza doria za Mitaa kwa kutumia magari na Pikipiki ambapo pia ameelekeza Kila Mkoa wa Kipolisi kutoa taarifa ya mwenendo wa Operesheni zitakazofanyika kila siku.

Aidha,  RC Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza msako wa kuwakamata wanunuzi wa mali za wizi huku akiwataka Wakuu wa Wilaya kuweka utaratibu mzuri wa kuanza kuwatumia Askari Mgambo lengo likiwa kuliongezea nguvu jeshi hilo.

Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa ananchi kuondoa hofu kwakuwa Serikali kupitia Jeshi la Polisi limejipanga kudhibiti uhalifu wowote.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema jeshi hilo limejipanga kutekeleza maelekezo ya RC Makalla ambapo amesema tayari wanawashikilia watuhumiwa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages