HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 10, 2022

BALOZI MULAMULA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS WA MISRI

 Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia  Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Abdel Fattah El-Sisi Jijini Cairo.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula aliwasilisha salamu za Mhe. Rais Samia kwa Rais El-Sisi, alisisitiza umuhimu wa kuendelea uhusiano wa kihistoria na ushirikiano katika sekta mbalimbali, za kimkakati hususan Ulinzi na Usalama, Elimu, Nishati na Mifugo. 

Aidha, baada ya mazungumzo na Mhe. Rais El-Sisi alikutana na kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Sameh Shoukri na kisha alifanya mahojiano na waandishi wa habari.

Moja wa Masuala ya msisitizo ni kuiunga mkono Misri kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mazingira COP27 utakaofanyika katika Jiji la Sharma Al Sheikh mwezi Novemba, 2022 na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika sekta za Afya, Elimu na nyinginezo kwa manufaaa ya Nchi hizi mbili.

Pia Balozi Mulamula alitumia mazungumzo hayo kuishukuru Misri kwa misaada mbalimbali inayoipatia Tanzania katika sekta za kimkakati pamoja na kuiunga mkono Tanzania katika mipango yake ya maendeleo kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Katika Mazungumzo hayo, Balozi Mulamula na Mhe. Shoukri walikubaliana kufanya Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) utakaofanyika Nchini Tanzania mwezi Desemba, 2022 baada ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (COP-27).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia  Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Abdel Fattah El-Sisi Jijini Cairo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia  Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Abdel Fattah El-Sisi Jijini Cairo.

 Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Mhe. Abdel Fattah El-Sisi Jijini Cairo akisoma Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia  Suluhu Hassan. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akifuatilwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dkt. Emmanuel Nchimbi. 

No comments:

Post a Comment

Pages