HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 15, 2022

Dk. SESEJA: BADO TUNAUHITAJI WA DAMU SALAMA LENGO NI KUPATA CHUPA 375,000

 Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. Best Magoma, Dk. Samweli Seseja akizungumza  katika kampeni ya Maadhimisho ya siku ya Uchangiaji Damu Duniani yenye kauli mbiu isemayo "Kuchangia Damu ni Kitendo cha Mshikamano, Tuungane Kuokoa Maisha.



Na Asha Mwakyonde, Dodoma


MPANGO wa Taifa wa Damu Salama haujaweza kufikia lengo la kukusanya chupa za damu ambazo zinakidhi mahitaji ya nchi nzima ambapo malengo ya mwaka 2022 ni kukusanya chupa 375,000 sawa na asilimia 70 ya mahitaji yote.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma Juni 14 na Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. Best Magoma, Dk. Samweli Seseja katika kampeni y Maadhimisho ya siku ya Uchangiaji Damu Duniani yenye kauli mbiu isemayo "Kuchangia Damu ni Kitendo cha Mshikamano, Tuungane Kuokoa Maisha (Donating blood is an act of solidarity. Join the effort and save lives), amesema  mahitaji kwa mwaka 2022 ni chupa 550,000 ambayo ni asilimia 1 ya idadi ya wananchi kwa makadirio ya takwimu za mwaka 2020.

 Dk. Seseja amesema kuwa  ripoti ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama imeonesha kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021 kwa kushirikiana na timu za halmashauri wameweza kukusanya chupa za damu 331,279 ambayo ni sawa na asilimia 88 ya lengo na asilimia 60 ya mahitaji ya nchi kwa kutumia vigezo vya  Shirika la Afya Duniani (WHO).

Ameongeza kuwa malengo ya kampeni kwa mwaka huu ni
kuwashukuru wachangiaji damu na kujenga uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu wa hiari wa kujirudia bila malipo.


"Nchi inahitajika kukusanya damu asilimia 1 ya wakazi wake au chupa 10 kwa kila wananchi 1000 na kwa hapa nchini tumefikia chupa 6 kwa kila watu 1000," ameeleza Dk. Seseja

Amefafanua kuwa  wahitaji wa damu nchini ni watoto chini ya Umri wa miaka mitano akina mama wakati wa kujifungua
wagonjwa wenye Saratani, Sikoseli, Virusi Vya UKIMWI na magonjwa wengine pamoja na wahanga wa ajali.

"Kama mwana jamii  yatupasa kuona umuhimu wa kujitoa kwa hiari kuchangia damu katika kipindi chote cha mwaka ili kuweza kufanikisha uwepo wa damu  ya kutosha kwenye vituo vyetu vya afya," amesema Dk. Seseja

Amesema mwananchi anapochangia damu anaonyesha mshikamono na anatoa zawadi ya uhai kwa mtu anayehitaji damu katika jamii yake.

Dk. Seseja ameongeza kuwa jamii inaweza kusaidia uwepo wa damu katika hospitali zao na kwa muda wote katika kampeni hiyo  kwa kufanya hivyo itasaidia kuokoa maisha ya mgonjwa mwenye uhitaji.

Ameeleza kuwa Maadhimisho hayo yamelenga kuwashukuru wachangia damu na kukuza uelewa na umuhimu wa kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

Kwa upande wake mchangiaji damu mkazi wa Dodoma Doto Shilogile amewahamashisha wananchi kujitolea kuchangia ili kuweza kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

" Kundi langu la damu ni 0 Negative ambalo ni kundi adimu kihistoria nimeanza kuchangia tangu mwaka 2005 kwa mwanafamilia na baadae kwa mke wa mkuu wangu wa kazi ambaye alijifungua na kupoteza damu nyinyi," amesema

Ameongeza kuwa safari yake ya uchangiaji damu ilianzia hapo hadi sasa kadi yake ya awali imeshajaa hivyo anahitaji nyingine ili aweze kuendelea kuchangia.

No comments:

Post a Comment

Pages