Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja mara baada ya kuwasili wilayani juzi mkoani Manyara kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Na Dotto Mwaibale, Hanang'
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru
Mwaka 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma ameweka Jiwe la Msingi kwenye miradi na
kufanya ukaguzi wa miradi hiyo yenye gharama ya zaidi ya Sh. Bilioni moja..
Akizunguza juzi Juni 17,2022 wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Mkuu wa Wilaya
Hanang' Janeth Mayanja aliitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Maji Gidangu -
Gidahababieg wenye thamani ya Tsh 120m, Mradi wa ujenzi wa madarasa manne
Nangwa Sekondar wenyei thamani ya Sh 84
Milioni, mradi wa ujenzi wa jengo la dharura Hospitali ya Tumaini wenye thamani
ya Sh 300 Milioni, ujenzi wa madarasa mawili Ganana Sekondari wenye thamani ya Sh 38 Milioni, mradi wa
ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami Barabara ya Mkapa wenye thamani ya Sh.
499 Milioni na mradi wa kikundi cha Vijana
Dream Studio and Stationery wenye thamani ya Sh 15 Milioni wa Kata ya
Katesh.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Geraruma ameridhika na utekelezwaji wa
miradi yote sita aliyoitembelea na kuikagua ambapo aliithibitisha na kutoa
pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja na Taasisi zote za Serikali
zilizopo wilayani humo kama Ruwasa, Tarura, Halmashauri na wananchi kwa
kutekeleza miradi hiyo kwa viwango.
Geraruma alitumia nafasi hiyo kuwahimiza watumishi wa Umma kusimamia miradi yote inayotekelezwa kwa wakati na kuzingatia miongozo.
No comments:
Post a Comment