Na Mauwa Mohammed Zanzibar
Kamati
ya Baraza la Wawakilishi imeishauri Serikali kusimamia vyema matumizi ya
fedha za umma ili watu wote wapate hamasa za kulipa kodi kwa hiyari na
hatimaye uwe ni utamaduni wa kulipa kodi bila shuruti.
Kauli
hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Baraza, Miraji Khams Waziri,
wakati akiwasilisha maoni ya kamati ya bajeti ya Baraza la Wawakilishi
kuhusu mwelekeo wa hali ya uchumi mpango wa maendeleo na bajeti ya
serikali kwa mwaka 2022/2023.
Mjume
huyo alisema lengo la ulipaji wa kodi kwa hiari litafikiwa pale ambapo
hakutakuwa na ubadhilifu katika fedha za umma na ukitokezea wahusika
wana wajibishwa bila muhali.
Aidha
kamati hiyo imeishauri serikali iweke mkakati malum wa kufuatilia
mapato yanayoweza kupatikana katika sekta ya mawasiliano kwani serikali
hukosa mapato mengi kutoka katika sekta hiyo.
Pia
kamati hiyo imetaka kila mamlaka ya serikali za mitaa kuainisha
vyanzo vyake vya mapato kwa uwazi kwani baadhi ya vyanzo vyengine
havikusanywi kabisa katika baadhi ya mamlaka ya serikali za mitaa lakini
vyanzo hivyo hivyo vinakusanywa na mamlaka za serikali za mitaa
nyengine.
Hata hivyo
kutokana na mwenendo wa hali ya dunia kamati hiyo ya baraza la
wawakilishi la Zanzibar imeishauri serikali kubuni mikakati mahsusi ya
kukabiliana na mitikisiko ya kiuchumi ya kidunia.
Alifahamisha kuwa mitikisiko hiyo mara nyingi husababishwa na vyanzo mbali mbali ikiwemo maradhi ya mripuko na vita.
Pia
kamati hiyo ilipendekeza kuimarisha huduma za jamii pamoja na
kuimarisha mifumo ya kielekroniki ya ukusanyaji mapato ya serikali.
Kudhibiti
matumizi ya serikali yasiyokuwa na tija ,kuimarisha utawala bora pamoja
na kuinua maslahi ya umma na kutekeleza miradi ya kimkakati.
Aidha
kamati hiyo ilisema ili kupatikana ufaniai wa tija katika utekelezaji
wa miradi ya kitaifa ni lazma kuwepo na vipaumbele kama vile kwa mwaka
2020/2023 kuliuwepo na vipaumbele vya kitaifa kama vile kusimamia
matum.izi sahihi ya ardhi na kupima maemeo yote.
Kikao cha baraza la Wawakilishi mkutano wa saba unaendelea huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar .
No comments:
Post a Comment