Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Yahaya Samamba akizungumza kuhusu tume hiyo.
Na Mwandishi Wetu
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa,
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan
imetilia mkazo ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini
(Local Content) na wajibu wa makampuni ya madini kutoa huduma kwenye
jamii inayozunguka migodi (CSR).
Mhandisi
Samamba ameyasema hayo leo Juni 02, 2022 katika Ofisi za Tume ya
Madini Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na baadhi ya vyombo vya
habari kuhusu fursa zilizopo kwa Watanzania kwenye Sekta ya Madini.
Amesema
kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya fedha zinazowekezwa katika Sekta ya
Madini zinakwenda kwenye maeneo ya manunuzi na kutoa huduma kwenye
masuala ya Ushirikishwaji wa Watanzania kwenye Sekta ya Madini (Local
Content) na kwenye miradi ya kijamii (CSR)
“Nachukua
fursa hii kuwaambia Watanzania wenzangu hasa vijana kuhakikisha kwamba
tunachangamkia fursa zilizopo katika utoaji wa huduma katika kampuni za
madini (Local Content) kwa maana ya manunuzi, ajira, mafunzo na
teknolojia inayopatikana kupitia uwekezaji kwenye Sekta ya Madini.
Ameeleza
kuwa, Serikali iliyopo madarakani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia
ilani yake ya mwaka 2025 iliahidi kutoa ajira kwa vijana na Watanzania
kwa ujumla na kuwataka kuchangamkia fursa zilizopo nchini.
“Ajira
hizo ni pamoja na kutoa huduma ya chakula, ulizi, huduma ya usafi
kwenye migodi , huduma za baruti, na kuuza vipuli ambapo zaidi ya
asilimia 80 ya watanzania wanatakiwa kuendesha mitambo ya kuchoronga,
kupakia vifusi vya mchanga wenye madini na kupeleka kwenye maeneo ya
uchenjuaji, amesema Mhandisi Samamba”
Ameeleza
kuwa lengo la serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa vijana na
wananchi wake na kuhimiza kuchangamkia fursa za kupata mikopo nafuu
kwenye Taasisi za Fedha pamoja na kupata maelezo zaidi ya nafasi, ajira
na fursa zilizopo kwenye migodi katika Ofisi 31 za Tume ya madini
zilizopo nchini.
Katika
hatua nyingine, Mhandisi Samamba amesema kuwa kupitia filamu ya Royal
Tour iliyotengenezwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la
kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini na kujitangaza kimataifa,
imeweka mazingira mazuri kwa Watanzania kwa ujumla kutumia fursa hiyo ya
kuwakaribisha wawekezaji na kushirikiana nao kwa uaminifu ili kunufaika
na Sekta ya
Aidha,
Mhandisi Samamba amesema kuwa, Serikali inaelekeza jamii inayozunguka
migodi kukaa pamoja na wawekezaji ili kuibua miradi ambayo inaigusa
jamii moja kwa moja kama vile miradi ya maji , elimu na mingine
inyozunguka migodi.
“Tuna
mafanikio makubwa katika maeneo hayo ambapo tuna miradi mikubwa katika
mkoa wa Geita kama vile barabara za lami, mashule, hospitali na mradi
mwingine wa Bulyanhulu uliojenga zahanati nzuri za kisasa katika Wilaya
ya Kahama na Halmshauri ya Msalala ambapo maeneo yote haya jamii imeweza
kunufaika na (CSR), amesema Mhandisi Samamba”
Katibu
Mtendaji amemalizia kwa kusema kuwa jamii inanufaika hata baada ya
miradi ya uchimbaji wa madini kuisha kwa kuwa inakuwa imezikuza sekta
nyingine kama vile biashara na kilimo.
No comments:
Post a Comment