Na WMJJWM, Dodoma
Katibu
wa Wabunge vinara wa Ustawi wa Jamii Mhe.Justine Nyamoga amesema wapo
tayari kushirikiana na Serikali kukemea vitendo vya ukatili kwenye
jamii.
Mhe. Nyamoga
ameyasema hayo Jijini Dodoma Juni 21, 2022 katika kikao kazi cha
kuwajengea uwezo wabunge vinara wa Ustawi wa Jamii kuhusu utekelezaji,
uendeshaji na usimamizi wa Afya mbalimbali za Ustawi wa Jamii katika
ngazi ya Halmashauri.
"Sisi
wabunge vinara tunawajibu wa kuwa mfano kwa Jinsi ambavyo tunaenenda
Kwa kukataa vitendo vya ukatili na kupaza sauti kuhusu vitendo hivyo
popote tutakapokuwa iwe ndani au nje ya Bunge katika kuiunga mkono
Serikali yetu" amesema Nyamoga.
Nyamoga
amepongeza pia hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda
Wizara inayohusika na Masuala ya Ustawi wa Jamii pamoja na kuridhia
katika ajira zinazotarajiwa kuwepo na Maafisa Ustawi wa Jamii ambapo
amesema itasaidia kuondoa mkanganyiko uliokuwepo na kuimarisha utendaji
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akifungua kikao hicho, amewapongeza wabunge Kwa
hatua ya makusudi kuamua kuunda kikundi cha vinara kwa ajili ya kusaidia
Jamii katika suala la ukatili wa kijinsia kuhakikisha unakwisha.
Mhe.
Mwanaidi amewaomba wabunge hao kutoa elimu kuhusu ukatili wowote na
madhara yake na kuwaeilimisha wananchi kushiriki katika kutoa ushahidi
mahakamani kwa wanaokabiliwa na vitendo hivyo.
Ameongeza
kwamba bado kuna upungufu wa Maafisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri
hali inayochangia utoaji wa Huduma za Ustawi kutopatikana kwa urahisi.
"Huduma
za Ustawi wa Jamii zinahitaji kufikia Jamii na Makundi yenye mahitaji
Maalum kwa wakati ili kutatua changamoto zinazowakabili ili washiriki
kikamilifu katika Ustawi na Maendeleo ya Taifa, hata hivyo kuna idadi
ndogo ya Maafisa Ustawi wa Jamii wanaopaswa kusaidia na kutoa huduma
hizo" amesema Mhe. Mwanaidi.
Akizungumza
katika kikao hicho Mkurugenzi wa Afya, lishe na Ustawi wa Jamii kutoka
Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe amewashukuru wabunge vinara
kwa kuisaidia Serikali kusukuma mbele masuala ya Ustawi wa jamii tangu
kikundi cha wabunge hao vinara kianzishwe mwaka 2021.
Dkt
Kapologwe amesisitiza uhitaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii ni mkubwa na
kwamba Serikali inazingatia na kulipa uzito suala hilo.
"Katika
kibali cha ajira ambacho tutaajiri watumishi wa Afya 7612 ndani yake
Kuna Maafisa Ustawi wa Jamii na Maaafisa lishe ambayo itasaidia sana
kupynguza changamoto iliyopo" amesema Dkt. Ntuli.
Aidha
amesema kupitia ajira zilizopitishwa na Mhe. Rais matarajio ni kuwa
Maafisa Ustawi wa Jamii katika vituo vyote vya kutolea Huduma za Afya
kwenye kila Halmashauri ambayo itasaidia kupambana na vitendo vya
ukatili na Masuala ya ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira
magumu na mimba za utotoni.
Awali
akieleza lengo la kikao hicho Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu
wa Ustawi wa Jamii Joseph Kahinga amebainisha kwamba wabunge wakipata
uelewa wataweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utekelezaji wa
Huduma za Ustawi wa Jamii kwa kupaza sauti katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment