WAZIRI
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy
Gwajima amesema katika stadi za ujasiriamali Vazi la Batiki litawekewa
viwango ili mtu yeyote duniani akishika vazi hilo litambulike kuwa ni
Batiki kutoka Tanzania.
Waziri
Gwajima ametoa kauli hiyo wakati wa Siku ya vazi la Batiki ambayo
imefanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam wakati wa
Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea.
"Tunataka
mahali popote vazi hili la Batiki mtu akilishika ijulikane kuwa ni
Batiki ya Tanzania kwani ni kwa njia hiyo tutaweza kuwakomboa watu wetu
na Umasikini" amesema Dkt. Gwajima.
Ameongeza
luwa lengo ni kuwafikia watengenezaji wa Batiki wakiwemo Wanawake
walio wengi kwenye Sekta ya Biashara ndogo ndogo ili kila mmoja aweze
kuinuka kiuchumi.
Dkt.
Gwajima amesema kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan amefungua fursa kwa
Wanawake na kuwaonesha kuwa wanaweza, hivyo nimuhimu kuchapa kazi kwa
kushirikiana na Wanaume kuinua Uchumi wa Nchi.
"Kutungwa
kwa Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 2018
inayozitaka Halmashauri zote kutenga 10% ya mapato yake ya ndani kwa
ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa makundi maalum ikiwemo wanawake
imewasaidia wengi ambapoMwaka 2020/21 zilitengwa jumla ya Sh. Bil. 62.68
na kufikia 30th Juni, 2021 Sh. Bil. 53.81 zilikopeshwa kwa Vikundi
7,993 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu sawa na asilimia 86"
alisema Dkt. Gwajima.
Amebainisha kuwa, kati ya Fedha hizo Sh. Bil. 28.17 zilitolewa kwa vikundi vya wanawake 4,894 vilivyozalisha ajira 52,428.
Kwa
upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe amewahimiza waandaaji wa Siku ya Batiki
kufanyika nchi nzima.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum, Zainab Chaula ameahidi kushirikiana na Katibu Mkuu wa
Zanzibar kufanyia kazi maelekezo ya Mawaziri hao.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TanzaniaBi. Latifa Mohamed Khamis,
aliomba Serikali kuhakikisha Shirika la Viwango nchini TBS, wanatoa
Vyeti vya Ubora wa Bidhaa za Batiki.
Awali
Mkurugenzi wa Taasisi Roijok Progress Centre, Rose Urio amesema kuwa
Uzinduzi huo ulikuwa na lengo la Kuitanga Batiki ndani na Nje ya Nchi.
Amesema
uzinduzi huo utafungua Masoko ya Batiki pamoja na akuwaunganisha
wazalishaji wa Batiki Tanzania kuwa na masoko ya ndani na nje ya Nchi.
"Tumefanya hii kwa msaada Mkubwa wa Serikali, tumekuwa na Viongozi wa Serikali ambao wamekuwa sababu kubwa ya sisi kufikia hapa.
Amesema
kuwa Maisha yamebadilika thamani ya mwanamke ni kuweza kujitegemea
kiuchumi ingawa Manamke anamajukumu makubwa ya kulea familia,
lakini Mapinduzi Makubwa yaliyotokea dunia hivyo mwanamke anakila sababu
ya kuingia kwenye uchumi.
Amesema Batiki ni
bidhaa inayoweza kuzalishwa hata eneo dogo lenye uwazi. "Kwahiyo sisi
Kama Roijok kupitia mradi wetu wa Batiki utasaidia kuanzia wazalishaji
wadogo mpaka wenye Viwanda."
Amesema Lengo ni wanawake kuweza kuzalisha lakini pia kusimamia Familia.
Amesema
katika Mradi wa Batiki wanampango wa kuzindua Ua la Mama ambalo
litakuwa kwaajili ya Kumuenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassani.
No comments:
Post a Comment