Rais wa Rwanda Paul Kagame (64) amebainisha kuwa anatarajia kugombea tena nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2024.
Kagame ameyasema hayo katika mahojiano maalum aliyofanya na kituo cha habari cha France 24 ambapo amenukuliwa akisema “nafikiria kugombea kwa miaka mingine 20 na sina tatizo na hilo, uchaguzi unahusu Watu kuchagua.”
Kagame ambaye alianza kuiongoza Rwanda akiwa na miaka 36, alibadilisha katiba ya nchi hiyo mwaka 2015 na kumruhusu kubakia madarakani hadi 2034 ambapo katika Uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2017 alifanikiwa kupata ushindi wa asilimia 99 ya kura.
No comments:
Post a Comment