Na Mwandishi Wetu
Benki ya NMB imeendelea kujidhatiti kibiashara na kujiimarisha kulihudumia taifa kupitia mtandao wake wa matawi ambao sasa umefikia matawi 227 kufuatia uzinduzi wa tawi la NMB Buhongwa mkoani Mwanza.
Akizungumza kabla ya ufunguzi rasmi wa tawi hi hilo Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw. Filbert Mponzi, alisema kati ya mwaka 2019 na 2021, NMB iliisaidia serikai kukusanya mapato yenye thamani ya TZS trilioni 8.6.
Akifafanua mchango wa NMB katika juhudi za maendeleo za serikali, Bw. Mponzi alisema sasa hivi Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) una zaidi ya taasisi 1,100 zilizounga mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato.
Aidha alisema kuwa pamoja na mtandao mpana wa matawi, pia NMB imeendelea kutumia tekinolojia kufikisha huduma zake kwa watanzania wengi zaidi na kulihudumia taifa kwa ujumla.
Bw. Mponzi alisema tawi hilo jipya ambalo ni la 13 mkoani Mwanza na 38 Kanda ya Ziwa, ni tawi kamili lenye huduma zote za kibenki, zikiwemo zile za mikopo kama kuwakopesha wakulima.
NMB imekuwa mstari wa mbele katika jitahada za serikali za kuimarisha kilimo nchini na tayari imetoa mikopo ya kilimo ya TZS bilioni 100 kwa riba nafuu.
Tawi hili la NMB Buhongwa ni tawi kamili lenye huduma zote za kibenki yaani huduma za miamala, mikopo, ushauri, kufungua akaunti, kufanya huduma za kubadiri fedha za kigeni, huduma za bima na hata ushauri wa masuala ya biashara na fedha,” Bw Mponzi alinena na kuongeza:
Kwa upande wake Mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo ya uzinduzi Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Sauda Msemo, alisema kuwa, NMB Pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi hadi vijijini kupitia matawi, vituo vya huduma na mawakala, ni mshiriki na mdau muhimu katika juhudi za Serikali za kuboresha huduma za kijamii kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbaili hasa za elimu na afya.
Naibu Gavana huyo pia aliipongeza NMB kwa kutenga zaidi ya 200 bilioni kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwenye sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
No comments:
Post a Comment