HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2022

Mwalimu Benki yaendelea kutoa mikopo Sabasaba

 Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko cha Benki ya Biashara ya Mwalimu, Leticia Ndongole (kushoto), akizungumzia namna walivyojipamga kutoa huduma kwa watu wote watakaotembelea banda lao ndani ya maonesho ya 46 ya biashara maarufu kama Sabasaba.

Timu ya wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya Mwalimu wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya viwanja vya maonesho ya 46 ya Biashara maarufu kama Sabasaba.

Wananchi wakitembelea banda la maonesho la Benki ya Biashara ya Mwalimu ili kupata huduma kwenye maonesho ya 46 ya Biashara maarufu kama Sabasaba.
 

Na Irene Mark

ZAIDI ya watanzania 50 waliotembelea banda la maonesho la Benki ya Biashara ya Mwalimu (MCB), wamepata mikopo huku wengine zaidi ya 35 wakifungua akaunti kwenye benki hiyo.

Baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea banda hilo namba 49 lililopo kwenye jengo la Jakaya Kikwete, katika maonesho ya 46 ya Biasahara maarufu kama Sabasaba walishuhudia umati wa wananchi wakipata huduma kutoka kwa watumishi wa MCB.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 7,2022 Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa MCB, Leticia Ndongole amesema wanatarajia idadi ya wakopaji na wateja wapya itaongezeka kwa kuwa huduma zinatolewa kwa watu wote.

“Tunaposema huduma tunatoa kwa watu wote maana yake ni walimu, wafanyabiashara, wanafunzi wa vyuo, wakulima, wafugaji, wasafirishaji, vijana na wazee... hatuachi mtu.

“Tunafungua akaunti za aina mbalimbali kwa hapa tumefungua akaunti 35 hivyo tunawakaribisha wote kuja kupata huduma zetu bora kwenye sekta ya benki.

“Kwetu hii ni mara ya kwanza kushiriki naonesho haya na tumeona tija yake na tunaahidi kuendelea,” anasema Ndongole.

Amesema walianza maonesho hayo Juni 28 na wataendelea kuwepo na kutoa huduma hadi Julai 13 mwaka huu yatakapohitimishwa rasmi.

Amesema wanatoa huduma kwenye mikoa yote hapa nchini kwenye matawi na kidijitali kupitia mawakala wa Mwalimu Benki, Mwalimu Mobile, Mwalimu Visa Card.

Amesema pia wateja wao hupata huduma zote za bima na mikopo ya vifaa mbalimbali vya ujenzi.

No comments:

Post a Comment

Pages