Mkurugenzi Mtendaji wa Global Educational Link Ltd,
Abdulmalik Mollel.
Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Aidha,
imewakumbusha watanzania kuchangamkia fursa za ufadhili wa masomo ya
vyuo vya nje zinazotolewa na vyuo vikuu vya nje ili wafaidike waweze
kupata elimu bora na viwango vinavyotambulika inayoendana na ushindani
wa soko la ajira la ndani na nje.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Educational Link Ltd,
Abdulmalik Mollel wakati akizungumza na wanahabari kwenye Ufunguzi wa
Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es salaam.
Mollel
amesema kuwa nchi ya Georgia ina idadi ya watu takribani milioni
nne,na kwamba inakumbwa na changamoto ya nguvu kazi kutokana na kuwa na
idadi kubwa ya wazee ukilinganisha na idadi ya vijana,hivyo wanafunzi
kutoka mataifa mengine ambao wanaenda kusoma kwenye nchi hiyo wanaweza
kupata ajira kirahisi baada ya kuhitimu masomo yao.
"Georgia
idadi ya watu takribani milioni nne,pia ni miongoni mwa nchi tajiri
duniani,nje tu ya kusoma kwenye nchi hiyo pia unapata ajira,kuna
changamoto ya nguvu kazi kwani wengi ni wazee,ili nchi yao iendelee
kupiga hatua wanahitaji nguvu kazi ,ili watoto wetu wanaosoma pale
wanaweza kuwatosheleza kwa ajira" amesema Mollel.
Amebainisha
kuwa wanafunzi wanaosoma kwenye nchi hizo za Ulaya wanaweza kupata Visa
ya Shengen ambayo inawapa fursa ya kuzunguka nchi zipatazo 30 ikiwemo
Italia, Ujerumani, Ufaransa, Hungary na Poland ambapo nchi hizo ni kubwa
zenye teknolojia kubwa lakini pia zina changamoto ya idadi ya watu
hivyo zinahitaji nguvu kazi.
"
Kwa wakati mwingine Global Education Link Ltd tumeona tuvilete Vyuo
Vikuu vya Ulaya hapa kwenye maonesho ili kuwasaidia vijana kuomba
kwenda kusoma kwenye nchi hizo, lengo letu siyo wanafunzi wanaenda
kusoma nje ya nchi warudi na chetu tu bali tunataka warudi na
wawekezaji,tunataka warudi na fursa ya Uwekezaji nakutusaidia kuajiri
vijana wenzao na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira" Amesema
Mollel.
Mkurugenzi huyo
ameongeza kuwa changamoto zinazowakumba vijana wakitanzania kukosa
ufadhili wa nafasi za masomo nje ya nchi ni pamoja na kuchelewa kutuma
maombi British Council hivyo kupelekea fursa waombaji wachache kupata
fursa hiyo,ambapo amewasisitiza watume maombi mapema.
Hata
hivyo ameongeza kwamba nchi ya India ina vyuo vya Elimu ya juu
vipatavyo 80,000 na kwamba ndani ya nchi hiyo kuna Vyuo vyenye kampasi
zaidi ya Moja vyenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 vikijitofautisha
na Vyuo vingine duniani
Kwa
upande wake, Meneja wa Kitengo Cha Mitihani kutoka British
Council-Tanzania, Henry Sangilwa amesema kuwa lengo la kuja kwenye
maonesho hayo ni kuwaletea habari njema za fursa za ufadhili wa masomo
zinazopatikana Nchini Uingereza.
Pia
amefafanua kuwa kila mwaka nafasi za ufadhili zipatazo 35 za wanafunzi
kwenda kusoma nchini humo hutangazwa lakini idadi ya watanzania
wanaojitokeza kuomba kwenda kusoma ni ndogo,hivyo amewasisitiza
kuchangamkia fursa hiyo ambapo dirisha la udahili litafunguliwa kuanzia
mwezi Agosti hadi Novemba.
" Vigezo vinapimwa kuanzia kuzungumza lugha ya Kiingereza ambapo hufanywa na British Council " amesema Sangilwa.
No comments:
Post a Comment