HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2022

Askofu Malekana awashauri Wanafunzi wa Elimu ya Juu kujiajiri baada ya kuhitimu


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Chuo Kikuu cha Arusha kinachomilikiwa na Kanisa la Waadventista (Wasabato)kimewashauri wanafunzi wote wanaotarajia kujiunga na Elimu ya  juu kusoma huku wakitambua changamoto ya ukosefu wa ajira siyo ya Tanzania pekee bali ya dunia nzima hivyo wanapswa kupata maarifa ya kujiajiri kupitia fursa za masomo wanazozipata

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Askofu Mark Malekana wakati akizungumza na wanahabari kwenye Ufunguzi wa  Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es  salaam. 

"Chuo chetu kina  falsafa yakipekee katika utoaji wa Elimu, tunamtayarisha Mwanafunzi  kiroho,kisaikolojia,kiuchumi na katika nyanja zote za maisha  kwa kufanya hivyo tunategemea mhitimu hata akikosa ajira atajiajiri mwenyewe bila kutegemea kuajiriwa"amesema Askofu Malekana.

Aidha amesema kwamba kupitia maonesho hayo wameamua kuzungumzia kwa kina na wazazi au walezi wanaofika kwenye Banda la chuo hicho kwenye viwanja vya Mnazi ili kuwashauri waweze kujiunga na masomo chuoni hapo wapate maarifa mazuri yatakayoweza kuwasaidia kujiajiri.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa chuo hicho, Elisha Lomay  amesema kuwa  wana falsafa ya kumjenga mwanafunzi akue katika maadili ya kiroho ,Kimwili, pamoja na kitaaluma ambapo wahitimu wengi wamekuwa wakifanikiwa kufanya kazi kwa weledi.

Amebainisha kuwa chuo hicho ambacho kinapatikana  Wilayani Meru Mkoani Arusha kimekua kikidahili wanafunzi bila gharama yoyote kupitia mtandaoni(Application fee bure) ,na kwamba baada ya wanafunzi kujiunga na chuo hicho wanalipia ada ambazo Wanaweza kuzimudu.

Aidha, amewakaribisha wazazi na walezi kuwaleta wanafunzi kwenye banda la chuo hicho la Maonesho ya TCU ili waweze kujengwa kitalauma kwa mwaka wa masomo 2022/23.

" Chuo chetu kinatoa ufadhili( Scholarship ) Kwa wanafunzi wanaotaka kusoma nje ya nchi kwa kushirikiana na wasabato wenzetu wanaoishi nje ya nchi ikiwemo Marekani,hivyo tunawakaribisha wazazi na walezi kuwaleta watoto wao kujiunga na chuo chetu kwani kina mazingira rafiki yakujisomea na gharama za ada na hosteli ni nafuu" amesema Lomay.

Amefafanua kuwa  programu wanazofundisha chuoni hapo ni pamoja na  Shahada ya Utawala wa Biashara na Uhasibu,Shahada ya Sanaa ya Ualimu, Shahada ya Sanaa ya Masomo ya Dini,Cheti na Astashahada ya Elimu ya Dini.

No comments:

Post a Comment

Pages