Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watu
wawili kwa tuhuma za mauaji huku likibainisha kuwakamata watuhumiwa nane
kwa makosa ya uhalifu.
Akizungumza na
wanahabari jijini humo Kamanda wa Kanda hiyo Jumanne Muliro amesema
katika tukio la kwanza wanamshikilia Selemani Haruna (24) mkazi wa
Kimara Temboni kwa mauaji ya binti wa kazi aitwaye Editha Charles.
Kamanda
Muliro amebainisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 6 mwaka huu
asubuhi ambapo alifika kwa kazi ya kuweka umeme kwenye nyumba ya Agatha
Stanlaus ndipo alipomshambulia binti huyo kwa kitu chenye ncha kali na
kwamba baada kutekeleza unyama huo alivunja mlango wa mwenye nyumba na
kuiba Sh 1.8.
Amesisitiza kuwa baada ya mauaji
mtuhumiwa huyo aliuficha mwili wa marehemu kwenye stoo ya nyuma hiyo na
kwamba kabla ya kufanya kitendo mtuhumiwa alikuwa akijua muda anaotoka
na kurudi nyumbani mwenye nyumba hiyo.
Ameongeza
kuwa jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na mtuhumiwa alipohojiwa
alikiri kuonyesha kiasi cha fedha Sh 6,000,000 kilichobakia baada ya
kununua simu na vitu vingine hivyo atafikishwa mahakamani.
Katika
tukio la pili, Kamanda Muliro amesema wanamshikilia mtuhumiwa Thomas
Ziganyike (71) Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mkazi wa
Mbezi Juu kwa kumpiga risasi mfanyabiashara.
Kamanda
Muliro amefafanua kuwa tukio hilo lilitokea Julai 9 mwaka huu ambapo
marehemu akiwa anaangalia kiwanja chao mtuhumiwa alitoka nje na kumpiga
risasi na kwamba walipofanya uchunguzi walikuta maganda manne ya risasi
na kwamba mtuhumiwa atapelekwa mahakamani.
Katika hatua nyingine, jeshi hilo linawashilia watuhumiwa sugu 8 kwa makosa ya uhalifu wa kutumia silaha.
Kamanda
Muliro amesema mtuhumiwa Jumanne Omari mkazi wa Mwikabe na wenzake 7
walikamatwa katika oparesheni kali dhidi ya uhalifu walikutwa na Runinga
nne, Kompyuta mpakato 2, Subwofer, simu za aina mbalimbali, vifaa vya
kuvunjia, visu, mapanga na bisibisi.
Pia amesema watuhumiwa hao wamekutwa gari namba T 787 DGW Toyota ambalo wanalitumia kubebea vitu vya wizi.
No comments:
Post a Comment