HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 21, 2022

MJENGO WA TADDEO LWANGA USIPIME

 

Mchezaji wa Kimataifa kutoka Uganda anayekipiga Simba SC Taddeo Lwanga (28) ameonesha picha mbalimbali za mjengo wake anao umiliki katika jiji la Entebbe Uganda.

Mchezaji huyo ameonesha picha hizo kwa lengo la kuwakumbusha vijana wote kwamba yeyote mwenye bidii anayo nafasi ya kutimiza ndoto zake siku moja na haijalishi itachukua muda gani kuzifikia.

Nyumba hii ya Lwanga ambaye ni Baba wa Watoto wawili ni ya gorofa moja na inapatikana Kajjansi barabara ya kuelekea Entebbe.

“Ni hisia za furaha na zisizoelezeka kumiliki nyumba hii” alisema Lwanga.




 

No comments:

Post a Comment

Pages