Kamati ya Maadili ya TFF imemuhukumu Msemaji wa klabu ya Yanga SC Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kipindi cha miaka miwili (2) na kutozwa faini ya Tsh. Milioni 20.
Adhabu hiyo inakuja kufuatia kitendo cha Msemaji huyo kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.
Adhabu hiyo inaanza leo Alhamisi, Julai 21, 2022.
No comments:
Post a Comment