NA TATU MOHAMED
WAZIRI
wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameiagiza
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kujenga jengo la kudumu ndani ya
viwanja vya maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (DITF) ili wananchi
waweze kupata huduma iliyo bora.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea
mabanda mbalimbali, Nnauye alisema ameshaongea na Mamlaka ya Biashara
Tanzania (Tantrade) kuwa TCRA ipewe ofisi ya kudumu ndani ya uwanja kwa
kuwa wanamajukumu makubwa kwa jamii.
Nnauye
alisema uwepo wa banda la kudumu la TCRA ndani ya maonyesho hayo
litarahisha wananchi kupata huduma kwa wakati, kupunguza gharama ambazo
zinatumiwa na mamlaka hiyo kila mwaka wakati wa maonyesho.
"TCRA
ni wadau muhimu kwa watanzania kama mtakuwa na jengo lakudumu mtaweza
kuwasaidia watanzania walio wengi kuweza kupata huduma sahihi"alisema
Nnauye.Alisema Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji hivyo mawasiliano yakipatikana katika ubora itaifanya Tanzania kuwa bora zaidi.
Aidha alisema licha ya kampuni za nje kuwekeze Tanzania, TCRA isisite kutoa huduma bora kwa watanzania.
"Pamoja
na huduma zote mnazotoa mtanzania anatakiwa apewe kipaumbele katika
suala zima la utoaji huduma hivyo hakikisheni mnawahudumia wananchi kwa
busara na upendo", alisema
Hata
hivyo Nape alivitaka vyombo vyote vya habari nchini kutangaza vitu
vizuri vilivyopo Tanzania ili kumuunga mkono Rais Samia Suruhu Hassan.
Vilevile aliwataka vyombo vya habari kulitangaza soko la ndani ili watanzania wavutiwe kuwekeza nchini .
Wakati
huo huo, alipotembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL)
amezitaka taasisi za Serikali kutumia teknolojia ya TEHAMA ya kuendesha
mikutano kwa njia ya mtandao (video conference).
Alisema TEHAMA hiyo itasaidia kupunguza gharama kwa serikali na itawawezesha kuwasiliana kwa urahisi zaidi kwa watumishi wao.
"Serikali ipo tayari kuwawezesha kutekeleza mpango huo wa TEHAMA, endelee kufanya kazi nzuri ya kuwahudumia watanzania," alisema
Naye
Mkurigenzi wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga alisema wao ndio wa kwanza
kutekeleza agizo la Serikali la kutumia njia ya mtandao yaani video
comfrence katika mikutano.
"Tuna wateja zaidi ya 10 mkoani Dodoma ambao tumeshawaunganishia huduma hiyo "alisema Mhandisi Ulanga
No comments:
Post a Comment