HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2022

NIC kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi nchi nzima

 


 

NA TATU MOHAMED 


KAMISHNA  wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) Dk. Baghayo  Saqware amesema serikali ipo tayari kushirikiana na Shirika la bima la Taifa (NIC)  kwa kuhakikisha inawafikia wakulima, wafugaji, na wavuvi wote  nchini.

Dk. Saqware ameyasema hayo jana alipotembelea katika banda la NIC lililopo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya kimataifa (DITF) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Amesema serikali imekuwa ikitegemea sana Shirika la  NIC katika kuendeleza soko katika maeneo ya bima ya kilimo, majengo, pamoja na bima mbalimbali.
Dkt Sqware amesema NIC ni wazoefu zaidi katika soko la bima kutokana na wao kuwa na mtaji mkubwa na wataalamu wa kutosha katika soko.

“Ukizungumzia bima Tanzania hakuna namna unaweza kuisahau NIC kwa maana ya wataalamu, uzoefu pamoja na mtaji,” amesema Dk. Saqware.

Vilevile amesema  hivi karibuni NIC wamejikita katika bima ya kilimo ambapo amewapongeza kwa hatua hiyo na kuhaidi kuendelea kushirikiana nao.

“Tayari tumewapatia namba viongozi wa NIC ili waweze kuwasiliana na  viongozi wa wakulima na wafugaji hapa nchini ili waaze kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuwafikia zaidi na kuwapatia bima," amesisitiza.

Naye Mkurungezi wa Masoko na huduma kwa wateja NIC, Yesaya Mwakifulele amesema katika Maonesho hayo NIC imejikita katika ushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha inatoa huduma mbalimbali kuhusu suala nzima la bima.

Amesema katika Maonesho hayo wamekuja na APP  ya NIC kigajani ambayo inamuwezesha mteja kupata huduma akiwa nyumbani bila ya kufika katika ofisi zao.

“Kupitia APP hiyo mteja anaweza kujihudumia kwa hatua chache tu ambayo ataweza kukata bima ya aina mbalimbali ikiwemo nyumba, gari.
 
Akizungumzia kuhusu suala nzima la madai amesema NIC imekuwa ikifanya  ulipaji huo   ndani ya siku saba tu iwapo  taarifa zote zikiwa sawa.

“Kwa sasa hatuna  madai yoyote ambayo ayajalipwa labda  yale ambayo taarifa zake aziko sawa,” amesema Mwakifulele.

Aidha amewataka  watanzania wote kwa ujumla  kufika  katika banda lao ili waweze kupata elimu pamoja na  huduma za uhakika za bima ambazo zitaweza  kumsaidia pale anapopata majanga.


No comments:

Post a Comment

Pages