Na Hussein Ndubikile, Dar
Chuo
kikuu cha Taifa Zanzibar(SUZA) kimewashauri Wazazi na walezi kuwaleta
wanafunzi katika banda lao la maonesho ya TCU ili waweze kupata fursa ya
kusoma kozi mpya ya Teknolojia Mawasiliano ya Umma katika mwaka wa
masomo wa 2022/2023.
Aidha
SUZA kimebainisha kuwa mwaka huu wa masomo kinatarajia kutoa wahitimu
wa mwanzo wa Shahada ya Uzamili wa Teknolojia ya Mawasiliano ya
Umma(IT)
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano na Masoko wa SUZA Khadija
Sadiq Mahumba wakati akizungumza na Wanahabari kwenye Maonyesho ya 17
ya Elimu ya Juu,Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu
Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Nchini( TCU)
Aidha
amesema kwamba chuo hicho kinatarajia kudahili wanafunzi wapatao 2000
Kwa programu mbalimbali zikiwemo za Elimu,Afya,Kilimo kwa ngazi
mbalimbali ikiwemo Cheti, Astashahada( Diploma) Shahada(Degree),Shahada ya Uzamili na Uzamivu.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Uhusiano na Masoko SUZA amesema kwamba Chuo
hicho kinatoa programu za Kozi za Utalii ambapo wanafunzi watakaosoma
kozi hizo watapata fursa ya kusoma lugha mbalimbali za kigeni ikiwemo
lugha ya Kireno,Kichina ,Kifaransa,Kijerumani,na kwamba chuo hicho pia
kinatarajia kuanza kufundisha Programu ya lugha ya Kikorea.
Hata
hivyo amebainisha kuwa wakati wa udahili wa dirisha la pili wanatarajia
kudahili wanafunzi kwa program mpya za Shahada ya Uzamili ya Benki na
Fedha( MSc Benking & Finance) pamoja na Shahada ya Uzamili ya
Utawala wa Fedha na Biashara ( MBA-Finance).
"
Ningependa kuwaomba wazazi wawalete wanafunzi kwenye banda letu hapa
Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam wajionee kozi tunazofundisha ili
wafanye maamuzi sahihi yakujiunga na chuo chetu chenye fursa ya kupata
ajira nje na ndani ya nchi" amesema Khadija.
No comments:
Post a Comment