Na Mauwa Mohammed, Zanzibar
Tume
ya Umoja wa Kitaifa ya UNDP imekutana na viongozi wa Chama cha ACT
Wazalendo kwa lengo la kutathmini hali ya kisisa na mwenendo
wa uchaguzi nchini Tanzania.
Mwenyekiti
wa Chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji alisema hayo mara badaa
ya kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi Kuu ya chama Vuga Mjini
Zanzibar.
Duni alisema
ujumbe huo umekuja kuangalia ni maeneo gani yanaweza kusaidiwa katika
chaguzi zijazo za mwaka 2025 ziwe huru na zenye kukubalika chini ya
usimamizi wa Tume huru ya uchaguzi.
"Umoja
wa Mataifa unaweza kutusaidi ili uchaguzi ujao uwe wa amani uwe huru na
wenye kuaminika katika mwenendo wa kuendeleza siasa za kidemokrasia
nchini "alisema Duni
Sambamba
na hilo ujumbe wa chama cha ACT Wazalendo umeleza hali halisi ilivyo na
kwamba wanahitaji kutekeleza maridhiano ya kweli yaliyokubaliwa na
marehemu Seif Sharif Hamad pamoja na Rais Hussein Mwinyi.
Nao
ujumbe huo wa UNDP ukiongozwa na mwakilishi kutoka umoja wa Mataifa
bibi Akinyeni Adegbola umesema watafikisha ripoti katika ofisi yao na
kueleza ni maeneo gani wataweza kusaidi ili chaguzi ziwe za amani huru
na haki.
No comments:
Post a Comment