Charles Polevich akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi wa jiji la New York.
Charles Polevich (72) amekiri kumuua baba mzazi wa Nicki Minaj kwenye ajali ya gari ambapo alimgonga na kuondoka bila msaada wowote Februari mwaka jana Jijini New York.
Polevich amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani na kutozwa faini ya dola za kimarekani elfu tano ($5,000) pamoja na leseni yake ya udereva kufungiwa kwa kipindi cha miezi 6.
Polevich amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani na kutozwa faini ya dola za kimarekani elfu tano ($5,000) pamoja na leseni yake ya udereva kufungiwa kwa kipindi cha miezi 6.
Alisema kuwa kwamba tangu tukio hilo litokee amekuwa akipata maumivu ya moyo na hakuna msamaha kwa tabia aliyoifanya.
Waendesha Mashtaka walisema, Polevich alimgonga Robert Maraj (64) ambaye alikuwa akitembea pembezoni mwa barabara na kisha kumuacha bila msaada wowote.
No comments:
Post a Comment