MKUU wa Wilaya ya Mbeya Dk. Rashid Mohamed Chuachua , akipokea hundi ya Shilingi Milioni 60 kutoka Meneja wa Benki ya NMB Kanda Nyanda za Juu Straton Chilongola akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ikiwa ni sapoti ya kuwezesha maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya mwaka huu 2022. Benki ya NMB ni mmoja ya wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ya NaneNane.
Benki
ya NMB imeendelea kuunga mkono serikali katika kufanikisha ufanyikaji
wa maonyesho ya sikukuu ya wakulima kitaifa (Nanenane) ambapo jana
imekabishi kiasi cha Sh. Milioni 60 kwa ajili ya maonyesho hayo.
Udhamini
huo unaifanya benki hiyo kufikisha kiasi cha Sh. Milioni 195 ambazo
imetoa kwa kipindi cha Miaka mitano katika kufanikisha shughuli za
manyesho hayo kitaifa.
Katika
hafla ya kukabidhi hundi ya fedha hizo iliyofanyika mjini Mbeya Meneja
wa NMB kanda ya nyanda za juu Kusini Straton Chilongola amesema kuwa
benki hiyo imetoa kiasi cha fedha kwa ajili ya kufanikisha shughuli
mbalimbali za maonyesho hayo.
“
Kwetu kusaidia sekta ya kilimo ni fahari yetu kwani kupitia kilimo,
benki hii imekuwa ikifanya biashara kubwa ambayo pia imechangia sana
ukuaji wa sekta ya kilimo nchini na Mbeya kwa ujumla,” amesema
Chilongola.
Amesema kuwa
kwa miaka mitano ambayo maonyesho ya Nane Nane yamefanyika nchini, NMB
imetoa udhamini wa zaidi ya shilingi milioni 195 fedha ambazo benki hiyo
inaamini zinachangia pakubwa katika kufanikisha maonyesho hayo muhimu
kwa taifa.
Aidha
Chilongola amesema kuwa katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Awamu ya
sita, Samia Suluhu Hassan, Mchango wa NMB kama benki wakujenga Uchumi
imara kupitia kilimo na ufugaji ni kuwa Ndani ya miaka minne, wamefungua
zaidi ya akaunti 644,034 za wakulima nchi nzima.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya ambaye alipokea hundi ya fedha hizo kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa huo Juma Homera aliishukuru Benki ya NMB kwa kutoa kiasi
hicho cha fedha ambacho alieleza kitawezesha maonyesho kufanyika kwa
ubora.
“Kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa, nawashukuru sana viongozi wa Benki ya NMB kwa udhamini wao,
tunaamini utatusaidia kuboresha maonyesho yetu,” alisema Dk.Chuachua.
Alisema
tayari maonesho hayo yameanza na hivyo kuwataka wananchi wakiwemo
wajasiriamali kutembelea mabanda na kwamba zipo kamati zinazoratibu
taratibu mbalimbali kwenye maonyesho hayo.
No comments:
Post a Comment