Na John Marwa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika CAF limemteua Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez kuwa Makamu wa Rais Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Klabu ya CAF na usimamizi wa mfumo wa leseni za Klabu.
Barbara Gonzalez ametajwa kwenye orodha ya Makamu wa Rais wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Klabu ya CAF na usimamizi wa mfumo wa leseni za Klabu kuanzia mwaka huu hadi 2024 akiwa chini ya Rais Ahmed Yahya atakaye ongoza Kamati hiyo.
Nafasi hiyo inaleta faida kwa Taifa la Tanzania katika maendeleo ya soka nchini nakujulikana zaidi kila kona ya Afrika.
Ni wazi mafanikio hayo yamechangiwa na ushiriki bora wa klabu ya Simba katika michuano ya Klabu ambako kwa misimu mitano iliyopita Simba wamefanikiwa kutinga Robo Fainali tatu, mbili za Ligi ya Mabingwa CAFCL na moja ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika CACC.
Faida nyingine inayopatikana ni kuwa na maamuzi katika mambo yanayohusu Soka la Afrika ambalo kama Taifa kumekuwa na uwakilishi Bora na ushidani Mkubwa kwa misimu ya hivi karibuni.
Barbara ni mwanamke pekee kwenye kamati hiyo chini ya Rais Ahmed Yahya ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mauritania.
Hii ni chachu ya kuwaibua watendaji na viongozi wa Soka Tanzania katika ngazi mbalimbali Ili kuwa sehemu ya kutoa mchango wa Maendeleo ya mchezo husika.
Nafasi kama hizi hazijitu kwa hisani bali ni kwa uwezo wa kiutendaji katika kusimamia mambo na matokeo yakapatikana kama ambavyo Barbara amethinitisha hilo tokea Simba wamemuamini na kumkabidhi kijiti cha kuiongoza klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment