Hati Fungani ya JASIRI ya Benki ya NMB Yashinda Nishani ya Platinum Upande wa Kundi la Dhamana Endelevu ya Mwaka Kwenye Tuzo za Mitaji kwa Wajasiriamali za Mwaka 2022 zilizofanyika Septemba 20, 2022.
Mhazini wa Benki ya NMB – Aziz Chacha (Kushoto) akipokea tuzo ya Hati Fungani Bora ya Mwaka 2022 kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Ufadhili wa Ujasiriamali (SME Finance Forum) - Mathew Gamser kwenye hafla ya tuzo iliyoandaliwa na Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa Wajasirimali Wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Nchi za G20, Shirika la IFC (mwanachama wa Benki ya Dunia) pamoja na Jukwaa la Kufadhili Ujasiriamali (SME Finance Forum) jijini Phnom Penh, Cambodia. Benki ya NMB kupitia hatifungani yake ya NMB Jasiri imeshinda tuzo ya ‘Platinum’ Upande wa Kundi la Dhamana Endelevu ya Mwaka Kwenye Tuzo za Ufadhili wa Ujasiriamali za Mwaka 2022.
Phnom Penh, Cambodia - Septemba 20, 2022
Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa Wajasirimali wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Nchi za G20, Shirika la IFC (mwanachama wa Benki ya Dunia) pamoja na Jukwaa la Kufadhili Ujasiriamali (SME Finance Forum) mwaka huu wameanzisha kipengele kipya cha Hati Fungani Endelevu ya Mwaka kuzitunuku Taasisi zinazofanya vizuri kwenye eneo hilo.
Hati Fungani ya NMB JASIRI ndiyo imechaguliwa kama mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo mpya. Ushindi huo umepatikana baada ya Hati Fungani hiyo kupitiwa na jopo la majaji zaidi ya 100 waliovutiwa na mlengo wake, muundo na uwezo wa kulihudumia kifedha kundi ambalo halizingatiwi kwa Mitaji ya kawaida iliyozoeleka.
Chanzo hiki cha Mtaji kinaendana vyema na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na Kanuni za Dhamana za Kijamii za Chama cha Kimataifa cha Masoko ya Mitaji.
Katika hotuba yake ya kukubali tuzo na heshima hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna, alisema: “Sisi NMB tumejitolea kuhakikisha tasnia ya fedha inachangia maendeleo ya Tanzania. Hati Fungani ya JASIRI yenye lengo la kupunguza pengo la Mitaji linalozikabili biashara ndogo ndogo na za kati zinazomilikiwa au kusimamiwa na akinamama ni keielelezo kizuri cha dhamira hii.”
Hati Fungani yetu imefanikiwa kupata matokeo yaliyotarajiwa ya kusaidia kuwawezesha wanawake kiuchumi na kushughulikia madhumuni matatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo ni lengo la kwanza, la tano na la kumi.
“Tuzo hii ni wakati muafaka wa kihistoria kwa sekta ya benki nchini, kwani inaiweka nchi yetu katika ramani ya dunia kwa uongozi kwenye Mitaji endelevu. Hati Fungani ya JASIRI inaweka kigezo kipya nchini na barani Afrika katika kukuza vyanzo vingine vya Mitaji mbadala kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na wakimataifa,” aliongeza.
Bi Zaipuna amesema tuzo hiyo ni kwa ajilia wa wafanyakazi wote wa NMB, washirika wake, wawekezaji na wasimamizi wa sekta ya fedha kwa kuchangia mafanikio makubwa ya dhamana ya JASIRI.
No comments:
Post a Comment