HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2022

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA AIPONGEZA UTT AMIS



Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala, wakati alipotembelea Makao Makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2022.

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (katikati) akiwa katika kikao na uongozi wa Kampuni ya UTT AMIS alipotembelea Makao Makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (katikati) akiwa katika kikao na uongozi wa Kampuni ya UTT AMIS alipotembelea Makao Makuu ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS, Simon Migangala (wa pili kulia), wakati alipotembelea ofisi za taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala UTT AMIS, Salmin Kaniki.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya UTT AMIS jijini Dar es Salaam.
 

 

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo, ameipongeza Kampuni ya UTT AMIS kwa utendaji mzuri katika majukumu yake ya kusimamia na kuendesha  mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.

 

Pongezi hizo amezitoa leo Septemba 6, 2022 wakati alipotembelea ofisi za kampuni hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam.

 

Akiwa katika ofisi za kampuni hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo alikutana na uongozi wa UTT AMIS na kufanya mazungumzo, ambapo aliipongeza menejimenti inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw.Simon Migangala kwa kuwawezesha watanzania kuweka akiba na kushiriki katika uwekezaji kwenye masoko ya fedha na mitaji.

 

Ikumbukwe kuwa UTT AMIS ni kampuni iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango,inaendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria ya masoko ya mitaji na dhamana ya mwaka 1994 pamoja na marekebisho yake na kanuni za mifuko ya uwekezaji wa pamoja za mwaka 1997.

 

UTT AMIS kwa sasa inasimamia mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni Umoja, Wekeza maisha, Jikimu, Watoto, Jikimu, Ukwasi na Hatifungani na huduma binafsi ya usimamizi wa mali.Kampui hii  mpaka sasa inasimamia rasilimali zenye thamani ya zaidi  ya shilingi Trilioni moja huku ikihudumia wawekezaji zaidi ya 200,000 waliopo ndani a nje ya Tanzania. Mifuko inayosimamiwa na UTT AMIS imekuwa ikitoa faida shindani ya kati ya 12%-14% kwa mwaka kutegemeana na hali ya soko.

 

UTT AMIS imeendelea kuboresha miundo mbinu yake ya tehama ili kuwarahisishia  wawekezaji kupata taarifa zao za uwekezaji kwa urahisi kupitia huduma ya SimInvest *150*82# .

Pia imeendelea kutanua wigo wa kuhudumia wawekezaji kupitia ofisi zake za Zanzibar, Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma. Vilevile Naibu Katibu Mkuu huyo  ameitaka UTT AMIS kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kunufaika zaidi na huduma za Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja.

 

No comments:

Post a Comment

Pages