HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2022

Serikali yaipongeza Benki ya CRDB kuandaa Tamasha la Elimu ya Bima



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Tamasha la Elimu ya Bima linaloendelea katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam. Mkuu huyo wa Wilaya aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa Tamasha hilo lenye lengo la kutoa elimu ya Bima kwa watumiaji wa vyombo vya moto kutokana na kwamba wamiliki wengi wa vyombo vya moto nchini hawana elimu ya kutosha kuhusu bima.
Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Benki ya CRDB, Moureen Majaliwa, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, alipowasili kwenye Tamasha la Elimu ya Bima lililoandaliwa na Benki ya CRDB.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe, akipata maelezo kutoka kwa Afisa Bima NIC
Insurance, Prosper Peter, alipotembelea banda la NIC kwenye Tamasha la Elimu ya Bima linaloendelea katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mteja (kati) akipata huduma katika banda la NIC.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, akiangalia vilainishi katika banda la ORYX Energies alipotembelea banda kampuni hiyo wakati wa Tamasha la Elimu ya Bima linaloendelea katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Kanda ya Pwani, Moses Mishinga.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, akizungumza na maafisa usafirishaji (Bodaboda) wakati wa Tamasha la Elimu ya Bima linalofanyika leo Septemba 17, 2022 katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo linaendelea katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa benki ya CRDB.

No comments:

Post a Comment

Pages