Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limewataka makocha wote wa Klabu za Championship kuwa na vigezo stahiki katika msimu wa Ligi' 2022/2023.
Hayo ni kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambayo imebainisha sifa na vigezo vya Makocha wanaopaswa kukaa kwenye mabenchi ya Klabu za Championship.
"Vigezo stahiki kwa Kocha Mkuu ni CAF B Diploma na Kocha msaidizi CAF C Diploma".
"Kila Kocha lazima awe na leseni inayotambuliwa na kutolewa na TFF Ili kuweza kukaa kwenye benchi. Kotokamilisha vigezo hivyo ni kosa kikanuni na hatua zitachukuliwa dhidi ya wale watakaokwenda kinyume." Imeeleza Taarifa hiyo.
"Makocha wote wnatakiwa kukamilisha taratibu zote za vigezo stahiki kufikia mwisho wa mwezi huu wa September." Imeongeza Taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment